Davido amepost picha Instagram aki hang pamoja na rapper wa Marekani ambaye pia ni baba wa mtoto wa muimbaji Ciara, Future.
Ukaribu baina ya wasanii wa Nigeria na mastaa mbalimbali wa
‘unyamwezini’ ni ishara kwamba muziki wa Afrika unaendelea kupenya
taratibu Marekani, japo kwa kupitia wasanii wa Nigeria zaidi.
Wiki hii pia tumeshuhudia Alicia Keys na mumewe Swizz Beatz
wakithibitisha kuwa ni mashabiki wakubwa wa Wizkid, kwa kupost video
Instagram wakicheza nyimbo zake.
Siku chache zilizopita Rihanna naye alionekana akicheza wimbo wa
msanii wa Nigeria, Timaya ambaye pia walipiga picha pamoja huko Barbados
katika tamasha la Cropover.
Drake naye aliamua kufanya remix ya ‘Ojuelegba’ ya Wizkid baada ya kuupenda mwenyewe.
Hii yote ni tafsiri kwamba muziki wa Afrika kwa ujumla umeanza
kuwaingia mastaa mbalimbali wa nje, na itasaidia kuutambulisha muziki wa
Afrika kwa ujumla hata kama ni kwa kupitia wasanii wa Nigeria.

Note: Only a member of this blog may post a comment.