Wednesday, August 12, 2015

Anonymous

NEC yatoa onyo kwa UKAWA na Wanasiasa, Hofu ya Ebola Rwanda, CCM kurudia kura za maoni? (Audio)

radio-mikrofon_01
Uchambuzi wa magazeti @Clouds fm umekupita? Nimekusogezea zile zote zinzoweka vichwa vya habari magazetini baadhi zikiwa na hizi kubwa.. 

Hofu ya ugonjwa wa Ebola ya tanda nchini Rwanda mmoja afariki dunia baada ya kuugua ugonjwa wenye dalili sawa na Ebola…Mamlaka ya mawasiliano TCRA imeendelea kuionya umma kuhusu matumizi mabaya ya mitandao ya kijamii haswa kipindi hiki kuelekea Uchaguzi mkuu. 

CCM kurudia kura za maoni kesho katika majimbo 5 nchini baadhi yakiwa Rufiji mkoa wa Pwani, na Kilolo mkoa wa Iringa…Dk. Wilbroad Slaa akana taarifa zinazosambaa kutoka kwenye account ya Twitter adai kuwa hajawahi kuwa na account hiyo. 

CCM na UKAWA gumzo…Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Martias Chikawe akanusha fujo zilizoambatana na msafara wa Edward Lowassa asema maandamano hayo kuelekea ofisi za NEC yalikuwa ya amani yaliofuata utaratibu wa kisheria. 

NEC yaionya UKAWA kutangaza matokeo ya Urais na pia imewaonya wanasiasa kuto kuingilia shughuli zao za Tume…Rais Jakaya Kikwete afanya uteuzi wa balozi mmoja na kubadilisha wengine 2 vituo vya kazi mmoja akiwa Wilson Masilingi anayekwenda Marekani na aliyetuliwa ni Charles Makakala anayekwenda kuwa Balozi wa Tanzania nchini Zimbabwe.
Sauti yote ya uchambuzi wa magazeti @Powerbreakfast ipo hapa chini.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.