Brighton Masalu
MSHINDI wa Big Brother Hotshots
2014, Idriss Sultan amesema licha ya kupata fedha nyingi aliposhinda,
lakini hivi sasa anaanza kuishiwa hivyo analazimika kuwa na nidhamu juu
ya matumizi yake ya fedha.
Akizungumza wakati wa hafla ya wasanii
na Rais Kikwete hivi karibuni, Idriss alisema mwanzoni aliziona kama ni
pesa nyingi, lakini kutokana na wingi wa majukumu na matumizi
mbalimbali, sasa anakiri ‘burungutu’ hilo linaanza kusinyaa kila
kukicha.
“Unajua pesa inayotumika haiwezi kubaki
kama ilivyo, kwa sasa lazima nikiri kuwa ni lazima niwe makini sana na
matumizi yangu, pesa inaanza kupungua, zamani nilikuwa nachukua bila
kuhesabu, lakini sasa hivi kila nikivuta droo ni lazima nihesabu,
‘zinakata’,” alisema Idriss huku akicheka.
Note: Only a member of this blog may post a comment.