DJ wa kike wa Nigeria na mtoto wa bilionea wa nchini humo, Femi
Otedola, aitwaye DJ Cuppy anatua Dar es Salaam wiki hii. Mrembo huyo
ambaye anakuja Dar akitokea Nairobi, Kenya yupo kwenye ziara ya
kuzunguka nchi takriban nane za Afrika.
Cuppy atatumbuiza Dar, Jumamosi hii.
Mfahamu zaidi Cuppy na baba yake bilionea, Otedola.
Femi Otedola ni CEO wa kampuni ya mafuta ya Forte Oil Plc mwenye
utajiri wa dola bilioni 1.2. Otedola ana watoto watatu wa kike akiwemo
Florence Otedola maarufu kama DJ Cuppy ambaye hufanya kazi ya UDJ jijini
London Uingereza.
Mwaka huu, DJ Cuppy ndiye aliyekuwa DJ rasmi kwenye tuzo za MTV MAMA
jijini London. Yaani yeye ndiye alikuwa akipiga muziki wakati wa tuzo
hizo. Damn!
Chini ni baadhi ya picha za DJ Cuppy akiwa na baba yake.
Note: Only a member of this blog may post a comment.