Huenda sasa Shilole anaweza kupata lepe la usingizi baada ya
mwanasheria maarufu nchini, Albert Msando kuahidi kumsaidia kufuatia
kupewa adhabu kali na baraza la sanaa la taifa, BASATA hivi karibuni.
BASATA lilimfungia muimbaji huyo wa ‘Nakomaa na Jiji’ kutojihusisha
na sanaa kwa mwaka mzima kutokana na kitendo chake cha kuidhalilisha
nchi alipokuwa akitumbuiza nchini Ubelgiji.
Shishi amepost selfie Instagram akiwa na Msando na kuandika,
“Nakuheshimu my kaka umeweza kujitoa kwa ajir yangu kwenye matatizo
yangu! Mungu atakulipa inshaaalah @albertomsando.”
Bongo5 imempigia simu Shilole kutaka kupata maelezo ya ni kwa vipi
mwanasheria huyo anamsaidia lakini amedai kuwa yeye si mzungumzaji wa
jambo hilo.
Msando ni mwanasheria wa watu wengi mashuhuri akiwemo Zitto Kabwe.
Note: Only a member of this blog may post a comment.