Thursday, August 20, 2015

Anonymous

Mtata ROSE NDAUKA: Nipo Tayari Kuolewa na Yeyote!

rose_ndauka_2012.jpg
ROSE Donatus Anjelus Ndauka ‘mtata’ amesema kama mwanamke aliyekamilika na mwenye kuhitaji heshima katika jamii, yupo tayari kuolewa na kuishi kama mama na mwanaume yeyote. 

Akichonga na Amani, Rose alisema japo mume bora anatoka kwa Mungu na kwamba anangojea aliye chaguo lake, lakini amechoshwa na hali ya kuishi bila ndoa.
“Mimi kama mwanamke ninayetoka kwenye familia yenye maadili, inafika wakati natamani kuishi katika ndoa, natamani kuwa na familia yangu na mume wangu na kwa sasa akitokea yeyote, nikajihakikisha kuwa anavyo vigezo ninavyovihitaji, hakika niko tayari kuanzisha naye safari ya maisha,” alisema Rose. 

Awali Rose alikuwa na uhusiano na msanii wa Bongo Fleva, Malick Bandawe ‘King Chiwaman’ na kufanikiwa kupata mtoto mmoja na mwishoni mwa mwaka jana waliachana.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.