Marapa Nicki Minaj na Meek Mill ambaye ni mpenzi.
New York, Marekani
WAKATI, marapa Nicki Minaj na Meek Mill ambaye ni
mpenzi wake wakitegemewa kumaliza ziara yao ya The Pinkprint waliyoianza
tangu mwezi uliopita,wameendelea kufanya vituko baada ya hivi karibuni
kokodi ukumbi kwa ajili ya kutazama muvi inayoitwa Staight Outta
Compton,wakiwa wawili tu.
Tukio hilo linalojenga vichwa vya habari kwenye anga la burudani kwa
sasa,lilitundikwa na Nick kwenye ukurasa wake wa Instagram baada ya
kuposti picha wakiwa wawili tu, yeye na Meek Mill kwenye ukumbi ambao
hakuutaja jina na kuambatanisha chini yake maandishi yaliyosomeka;“
Ni lini wewe na mpenzi wako mtakodi ukumbi mzima kuangalia muvi ya
Staight Outta Compton?” alimaliza Nick Minaj kwa kumsifia pia mmoja wa
waigizaji ambao wako ndani ya sinema hiyo akiwemo rapa Ice Cube

Note: Only a member of this blog may post a comment.