Watoto hao ni miongoni mwa mamia ya watu
wanye ulemavu wa ngozi nchini humo ambao wamekuwa wakiwindwa na watu
wanaotaka viungo vya miili yao kwa shughuli za kishirikina.
Watoto hao, ambao mmoja ni kike na wanne
wa kiume kutoka Mikoa ya Kaskazini Magharibi na Kusini Magharibi mwa
Tanzania, wamekuwa wakipata matibabu hayo katika hospitali ya watoto
Philadelphia Shriners Hospital iliyopo jijini New York, Marekani.
Tayari watoto wanne wamekwisha wekewa
mikono na miguu ya bandia, wakati yule aliyekatwa taya akitarajiwa
matibabu yake kuchukua muda mrefu zaidi.
Ofisa kutoka shirika la Under the Same
Sun Martin Haule amesema watoto wanaendelea vizuri na kwamba ni wenye
furaha na kwamba wanatarajiwa kurudi nyumbani Tanzania mnamo mwezi
Septemba.
Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa, ulemavu wa ngozi unaathiri takribani mtu mmoja katika kila watu 15,000 nchini Tanzania.
Watu hawa wanawindwa kwa ajili ya viungo
vyao, ambavyo vinatakiwa katika biashara haramu kwa matumizi ya
shughuri za kishirikina.

Note: Only a member of this blog may post a comment.