Jokate Mwegelo ‘Kidoti’.
SIKU chache baada ya
kupata ushindi wa Tuzo ya Muigizaji Bora wa Kike kupitia filamu ya
Mikono Salama, muigizaji Jokate Mwegelo ‘Kidoti’ amesema kamwe
hakubahatisha na kwamba ataendelea kuongeza bidii katika uigizaji wake
japo hajaweka nia thabiti juu ya kazi hiyo.
Akizungumza na gazeti hili kwa njia ya
simu hivi karibuni, mrembo huyo alisema, anaamini ana kipaji halisi cha
kuigiza, lakini kupata tuzo hiyo haimaanishi kuwa anajua kuliko wenzake.
“Hiki ni kipaji changu halisi, nashukuru
sana kwa kupata ushindi huu, sijabahatisha, wameangalia vigezo lakini
haimaanishi kuwa naweza kuliko wengine,” alisema Jokate


Note: Only a member of this blog may post a comment.