Gladness Mallya na Erick Evarist
INASIKITISHA! Wakati
mama wa staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Sanura
Kassim ‘Sandra’ akiendelea vizuri baada ya matibabu nchini India, naye
baba wa jamaa huyo, Abdul Jumaa ‘Baba D’ anateswa na kansa ya ngozi huku
mwanaye huyo akiwa hana habari naye.
Staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz.
BOFYA HAPA KUMSIKIA BABA D
Akizungumza na gazeti hili kwenye
mahojiano maalum nyumbani kwake, Magomeni-Kagera, Dar, baba Diamond
alisema baada ya kuugua miguu kwa muda mrefu na kumaliza fedha nyingi
kwenye hospitali tofautitofauti huku akichanganya na dawa za kienyeji,
hivi karibuni amegundulika kuwa ana kansa ya ngozi.
“Miguu imenitesa kwa muda mrefu sana
huku ikitoa magamba na maji. Hivi karibuni niliamua kwenda Hospitali ya
Ocean Road (Dar) na kugundulika kwamba nina kansa ya ngozi.
“Nateseka sana kwani kila baada ya siku
saba zinatakiwa shilingi laki nne (400,000) kwa ajili ya dawa, jambo
ambalo linaniumiza sana kichwa kwani gharama hizo zimekuwa ni mtihani
mkubwa sana kwangu kwa sababu sina uwezo,” alisema Baba D kwa huzuni.
Aliendelea kueleza kwamba, baada ya
kugundulika ana kansa aliwasiliana na mwanaye wa kike ambaye naye ni
msanii wa Bongo Fleva, Mwajuma Abdul ‘Queen Darleen’ ambaye
alimuunganisha na Diamond na kumweleza hali yake juu ya ugonjwa huo.
ATELEKEZWA HOSPITALINI
Alisema kuwa, baada ya kumwambia,
Diamond aliahidi kumsaidia katika suala zima la matibabu ndipo
akamwambia aende wakakutane katika hospitali hiyo ya Ocean Road.
“Nilienda Ocean Road kama tulivyoelewana
na mwanangu Diamond lakini kitu ambacho kiliniumiza ni kwamba nilikaa
pale namsubiri kuanzia asubuhi hadi jioni hakutokea, nikaamua tu kurudi
nyumbani na kuanzia siku hiyo ‘ameni-bloki’ kwenye simu.
“Kila nikimtafuta simpati na mwanzo
tulikuwa tukiwasiliana mpaka nikamtumia na namba ya simu ya daktari
wangu. Pia aliniahidi kama itashindikana atanipeleka nje ya nchi lakini
yote hayo yameishia hewani, juzi nikasikia amemfanyia sherehe ya
bethidei mama yake,” alisema Baba D.
OMBI LA BABA DIAMOND
“Naomba mama Diamond aniambie tu ukweli
kama huyo siyo mwanangu nijue kwa sababu nateseka jamani, maana
inawezekana alishamwambia mwanaye mimi siyo baba yake ndiyo maana
ananifanyia hivi au kama nilimkosea ni kosa gani hilo lisilosameheka?”
Alihoji Baba Diamond.
KANSA YA NGOZI
Ugonjwa unaomsumbua Baba Diamond wa
kansa ya ngozi ambayo huitwa Melanoma ni ugonjwa unaompa mtu mateso
makali kutokana na maumivu anayoyapata na matibabu yake yanahitaji
gharama kubwa mno.
Ugonjwa huu huweza kusambaa na kushambulia viungo vingine zaidi ya ngozi kama mifupa na ubongo.
Dalili za kansa ya ngozi ni pamoja na kubadilika kwa ukubwa, rangi au ule muundo wa alama ya ngozi ambayo mtu amezaliwa nao.
Kuna tiba nyingi za kansa ya ngozi. Kuna
zile za hospitali ambazo ni lazima zinunuliwe, lakini kuna tiba ambazo
kwa ushauri wa daktari hata wewe unaweza kuziandaa bila kutumia gharama
kubwa.
Moja ya tiba hizo ni kunywa maji ya moto
ambayo yanatibu magonjwa mengi ikiwemo figo, kutoa sumu mwilini,
kuyeyusha mafuta tumboni, kurahisisha mzunguko wa damu, kuondoa sumu
kwenye ubongo na kusafisha haja ndogo.
TUJIKUMBUSHE
Kabla ya kugundulika kuwa na kansa ya
ngozi, Baba Diamond aliwahi kuripotiwa kuwa hoi akisumbuliwa na maradhi
ya miguu ambapo pia alilalamika kutelekezwa na mwanaye huyo.
Hata hivyo, baada ya kelele nyingi za ‘midia’, Diamond alikubali kumhudumia kabla ya madai haya mapya kuwa ameingia mitini.
Diamond hakupatikana kufuatia namba yake
kutokuwa hewani na hata alipotumiwa malalamiko ya baba yake kwa njia ya
WhatsApp hakujibu.

Note: Only a member of this blog may post a comment.