NI Jumamosi nyingine Mungu ametujalia uzima na kuweza kunikutanisha na ninyi wasomaji wangu katika safu hii ili kuweza kukipata kile ambacho nimekuandalia wiki hii.
Bila kupoteza muda nianze kuichambua mada iliyopo mezani. Kwa utafiti usio rasmi, ulimwengu wa sasa watu wengi huoana wakiwa hawapendani.
Wanalazimika kuingia kwenye ndoa kutokana na sababu fulani. Wengi wanaoa au kuolewa kwa sababu tu wameshatangatanga huku na kule bila mafanikio.
Watu wa aina hiyo ukiwauliza kwa nini wameoana wakati hawapendani, watakwambia hawakuwa na jinsi. Huo ndio ukweli. Ukiwauliza wanaume wengi sasa hivi kama wameoa wake ambao walikuwa wanawapenda kwa dhati, jibu lao litakuwa ni hapana.
Watakwambia wameoa kwa sababu ya kupata ‘wife material’. Kwamba wameshahangaika sana kutulia na wanawake ambao mioyo yao inawapenda lakini bahati haikuwa kwao, hawakupendwa.
Wanaume hao wanakuwa wamewekeza nguvu nyingi za kupenda lakini wapi, wanaambulia maumivu. Wanawake wanaowaumiza, nao wanakuwa na wanaume wanaowapenda na hao wanaume wanaopendwa nao wanawapenda wanawake wengine kabisa tofauti na wao.
Huo ndio ukweli. Ukiwauliza wanawake wengi walioolewa kwa sasa pia majibu yao hayatatofautiana sana na wanaume niliowaainisha hapo juu.
Simulizi zao hazitofautiani sana. Wanawake wengi wanaingia kwenye ndoa wakiwa wameshawapenda wanaume wengine tofauti na waume zao lakini wakaambulia maumivu, wanaolewa ili kutimiza wajibu.
Wanaolewa kwa sababu na yeye aonekane ameolewa. Aliyemuoa yawezekana akawa mzee, akawa hajampenda lakini atafanyaje na umri unamtupa mkono? Anaolewa apate heshima na kufanyiwa sherehe.
Hafikirii sana kama ndoa ni kifungo, kwamba anayemuoa ataishi naye kwa muda wote wa maisha yake. Hana muda wa kumtathimini na kuwaza kwamba aolewe na mtu ambaye anampenda, anachohitaji ni ndoa kwa namna yoyote.
Hivyo ndivyo mambo yanavyokuwa. Wanaopendwa hawapendeki, wanapenda sehemu nyingine ambako nako hawapendwi.
Mwanaume anakuwa ana mwanamke mwingine ambaye anampenda lakini bahati mbaya mwanamke huyo naye anakuwa hampendi. Kila mmoja anapishana na penzi la kweli, anaangukia kwenye penzi ambalo si salama kutokana na kuusikiliza moyo wake.
Mwanaume hulazimisha penzi kwa mwanamke ambaye hana upendo hata chembe. Mwisho wa siku ukweli unabaki palepale. Anaambulia maumivu.
Kamwe huwezi kumbadilisha mtu ambaye tayari moyo wake haupo kwako. Zaidi hapo hakutakuwa na penzi, maumivu itakuwa ni sehemu ya maisha yako.
Uvumilivu huwa haudumu, unahangaika kupata suluhisho la moyo, humpati. Humpati kama yule aliyekuwa anakupenda na wewe humpendi. Matokeo yake sasa, unarudi kule kwa yule aliyekuwa anakupenda na wewe humpendi. Unamuoa. Unafikia uamuzi huo ukiwa huna jinsi. Umeshatangatanga vya kutosha, umri unakuwa umeshakutupa mkono na kuona bora uoe.
Ndoa ya namna hiyo inakuwa na changamoto zake. Moyo wako hauwi mweupe pindi unapokuwa na mwenzako. Hapo ndipo linapoibuka suala la kuwa na michepuko. Yule aliyeingia kwenye ndoa akiwa hajampenda mwenzake analazimika kutafuta furaha kwenye mtu anayempenda kwa kisingizio cha kufurahisha nafsi yake.
Upendo wa kweli kwa mkewe unapungua kama ‘ataigiziwa’ vilivyo kule anakopata burudisho la moyo. Migogoro ndiyo inaanza hapo na ndoa inakuwa ndoano.
Nini kifanyike?
Tengeneza mazingira ya aina ya ndoa unayoitaka. Ishi katika mazingira na tabia za muoaji au muolewaji. Muombe Mungu akuoneshe mke au mume ambaye utampenda na yeye akupende vivyo hivyo. Ndoa ya watu wanaopendana siku zote huwa na furaha maishani.
Ndoa zinazofungwa kwa sababu ya maslahi, umri kutokuwa rafiki au sababu nyingine zinazofanana na hizo huwa hazina furaha. Ni rahisi sana kuandamwa na migogoro ya kila kukicha pale mmoja wao atakapoanza kusaka furaha ya moyo wake nje ya ndoa.
Siku zote ndoa yenye furaha na amani ni ile ambayo kila mwanandoa anampenda mwenzake kwa dhati.
Tukutane wiki ijayo kwa mada nyingine nzuri!

Note: Only a member of this blog may post a comment.