IMEVUJA! Siri ya kitu
kilicho kichwani mwa Katibu Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo
(Chadema) Dk. Wilbroad Slaa kuhusu mustakabali wake wa kisiasa umedaiwa
upo kwa mkewe, Josephine Mushumbushi, Ijumaa Wikienda imevujishiwa.
Dk. Wilbroad Slaa.
Chanzo cha kuaminika kilicho karibu na
mwanasiasa huyo, kimeliambia gazeti hili kuwa mke wa kiongozi huyo
mwenye ushawishi mkubwa katika siasa za Tanzania, anafahamu uamuzi
uliochukuliwa na mumewe, isipokuwa kinachosubiriwa ni siku ya kutoboa
kwa Watanzania.
Alipotafutwa Dk. Slaa ili aweze kuzungumzia suala hilo, simu yake haikupatikana. Jitihada zinaendelea.
Sakata la Dk. Slaa na chama chake lilijitokeza baada ya Chadema
kumkaribisha waziri mkuu aliyejihuzulu, Edward Lowassa aliyejiunga na
chama hicho na kuteuliwa kuwania urais kupitia muungano wa Ukawa.

Note: Only a member of this blog may post a comment.