Imelda Mtema
MIRIAM Jolwa, maarufu kama Jini
Kabula, ambaye ni staa kutoka Bongo Movie, amemshangaa aliyekuwa mpenzi
wake, Ruta Bushoke kumkana kuwa hawajawahi kuwa wapenzi.
Akistorisha na gazeti hili hivi
karibuni, Kabula alisema maneno ya mkali huyo wa muziki wa Kizazi Kipya
yanaashiria kama mtu anayechanganyikiwa, kwani asingeweza kujinadi kuwa
ni mpenziwe kama haikuwa hivyo.
“Yaani inawezekana Bushoke anataka
kupata uchizi kwa kweli, hivi kuna mtu anaweza kujinadi kuwa ni mpenzi
wa mtu wakati siyo! Kwanza kwa kitu gani jamani? Nina wasiwasi naye
kwamba siyo mzima,” alisema Kabula.
Wiki chache zilizopita, Bushoke
aliyeimba kibao cha Mume Bwege, aliwahi kudai kuwa hakuwahi kuwa na
uhusiano wa kimapenzi na Jini Kabula.
Note: Only a member of this blog may post a comment.