Kwa mara ya kwanza leo hii katika historia ya Barclays Premier
League, mechi ya ligi hiyo imechezwa siku ya Ijumaa – hii imekuja baada
ya utaratibu mpya uliopangwa msimu huu. Vilabu vya Manchester Utd na
Aston Villa ndio wameufungua usiku wa mechi siku za Ijumaa. 
Mchezo uliochezwa katika dimba la Villa Park umemalizika kwa Manchester United kuendelea kuwatambia Villa uwanjani kwao.
Mchezo uliochezwa katika dimba la Villa Park umemalizika kwa Manchester United kuendelea kuwatambia Villa uwanjani kwao.
Ikumbukwe Villa hawajahi kupata ushindi dhidi ya United katika mechi 20 zilizopita.
Goli pekee la Adnan Januzaj katika kipindi cha kwanza lilihakikishia
United ushindi wa pili mfululizo katika kipindi cha siku 7 zilizopita.
Hii
ni mara kwanza kwa Manchester United kucheza mechi mbili za ufunguzi
bila kuruhusi goli tangu msimu wa 2005/06 – huku Sergio Romero
akionekana kuanza kuzoea kulinda lango la United.
Manchester United sasa wanaongoza ligi wakiwa na pointi 6, baada ya kucheza mechi 2.
Note: Only a member of this blog may post a comment.