Makongoro Oging’ na Haruni Sanchawa
HALI ni tete!
Matukio ya mauaji ya askari polisi sasa ni tishio. Hilo limebainika
kufuatia Mkuu wa Kikosi cha Kupambana na Majambazi Mkoa wa Morogoro, ASP
Elibariki Israel Palangyo (53) kuuawa kwa kupigwa risasi na watu wenye
harufu ya ugaidi, Uwazi limechimba.
Tukio hilo la lililoacha maswali mazito
kwa majirani, lilijiri Agosti 4, mwaka huu nyumbani kwake, Yombo ya
Kilakala wilayani Temeke jijini Dar ambapo ni siku chache tu baada ya
watu wanaosadikiwa kuwa ni magadii kuvamia Kutuo cha Polisi Stakishari,
Dar na kuua watu saba, wakiwemo polisi wanne.
ALIVYOUAWA
Simulizi za kidaktari zinasema kuwa,
watu hao walimvamia marehemu chumbani kwake, wakampiga risasi nne sehemu
ya moyo, wakamkatakata mapanga na kumtoboa macho.
Hayo yalifanyika huku binti yake aitwaye
Neema Elibariki ambaye ni mwanafunzi wa kidato cha tatu Shule ya
Sekondari Kibasila, Dar akishuhudia.
Akisimulia mkasa mzima tangu kuvamiwa mpaka kuuawa kwa baba yake na yeye kupewa msukosuko, Neema alisema:
Akisimulia mkasa mzima tangu kuvamiwa mpaka kuuawa kwa baba yake na yeye kupewa msukosuko, Neema alisema:
“Kwanza sikutegemea kuwa leo hii
ningemkosa baba kutokana na mauaji ya kikatili, kidhalimu na kinyama.
Hii ni hatari sana kwa usalama wetu sisi wananchi na polisi kwa ujumla.
Kama imetokea hali ya magaidi kupenya na kujiimarisha na kuanza mauaji
kwa kasi namna hii, usalama unatoweka.”
AANZA NA SIKU YA TUKIO
AANZA NA SIKU YA TUKIO
“Nakumbuka siku hiyo (Agosti 4) saa tisa
usiku, uvamizi ulitokea. Mji wetu uligubikwa na milio ya risasi.
Nilishindwa kupata jibu kwa haraka ni kitu gani kilichotokea, tulikaa
kimya.
“Kabla ya milio ya risasi tulisikia watu
wakiongea kwa sauti ya chini huku geti kuu alionekana mtu akifungua.
Ndipo wakaingia watu zaidi ya kumi wakiwa wamejifunika vitambaa vyekundu
usoni.
“Baadhi ya watu hao walikuwa na bunduki, wengine mapanga. Walikuja moja kwa moja hadi mlangoni, wakavunja geti na mlango kisha wakafanikiwa kuingia sebuleni. Hawakujua pa kwenda. Baadaye waliingia chumba cha dada ambaye alikuwa amelala na mfanyakazi wa ndani. Waliamshwa wakanyang’anywa simu.
“Walipotoka huko, walihamia chumbani kwangu. Mimi nilikuwa nimelala na mdogo wangu. Ana umri wa miaka mitano. Wakatutoa sebuleni, wakamtishia mdogo wangu awaoneshe chumba cha baba. Mdogo wangu alifanya hivyo. Wakajaribu kubomoa mlango ikashindikana. Mmoja alitoka nje na kuchukuwa tofali, wakaupiga mlango ili ufunguke ikashindikana, wakapiga risasi komeo ikafunguka. Wakati huo walikuwa wametushikilia.
“Baba naye kumbe alishaamka. Alijua kuna uvamizi kutokana na ile milio ya risasi. Nilimsikia akipiga simu mahali kuomba msaada mara kwa mara lakini hadi anakufa hakuna aliyeweza kufika. Pengine waliogopa risasi.

Wale watu wakati wanaingia chumbani kwake, baba alikuwa ameshika panga, akamkata mkono yule wa kwanza kuingia.
“Walimpiga baba risasi za kifuani upande
wa kushoto kwa chini, akakimbilia chooni kujificha kwa kujifungia
lakini hakuweza, walimuwahi kwa kumpiga tena risasi huku wakimwambia
kuwa walichohitaji kutoka kwake ni uhai wake tu. Nilimwona baba
akiishiwa nguvu na kudondoka chini.”
AJARIBU KUITA WATU KWA FILIMBI
AJARIBU KUITA WATU KWA FILIMBI
“Kuona vile, nilipata ujasiri,
nilichukua filimbi ya kazini kwa baba, nikapuliza kwa lengo la kuita
watu waje kumuokoa baba, lakini walinipiga kofi na kunitishia kuniua.
“Niliamua kuingia uvunguni mwa kitanda
kujificha, mdogo wangu alichanganyikiwa, alikaa kimya maana hata yeye
alikuwa chumbani kwa baba. Walianza kuangalia vitabu, wakaangalia kitabu
cha mama na kukuta bahasha yenye shilingi laki tano na elfu arobaini,
wakachukua.”
MKE WA MAREHEMU ALIKUWA WAPI?
MKE WA MAREHEMU ALIKUWA WAPI?
“Mama yangu mzazi yeye ni muuguzi. Kwa hiyo wakati baba anauawa yeye alikuwa kazini kwake, Hospitali ya Zakhem, Mbagala (Dar).”
WAONDOKA, WAACHA MANENO
WAONDOKA, WAACHA MANENO
“Jambo la ajabu, licha ya kumuua baba,
waliendelea kufyatua risasi ndani. Lakini nje pia nilisikia milio ya
risasi. Inaonekana nje ya geti kulikuwa na kundi kubwa la wenzao ambao
pia walikuwa wakipiga risasi hovyo. Baada ya muda kukawa kimya, wale wa
ndani waliondoka huku wakisema watarudi tena kwa ajili ya kuvamia nyumba
nyingine iliyo jirani na yetu huku wakisema nchi itatikisika.”
KUMBE MAREHEMU ALIKUWA NA BASTOLA
KUMBE MAREHEMU ALIKUWA NA BASTOLA
“Baba alikuwa na bastola ndani lakini
risasi zilikuwa mbali. Nafikiri alishindwa kujua kwa haraka alipoziweka
lakini polisi walipofika walikuta risasi nje zilizofichwa. Mama alipata
taarifa lakini alikutana na polisi wakiupeleka mwili wa baba Hospitali
ya Temeke. Wahalifu hao walitoka na fedha lakini pia walifanikiwa
kuondoka na simu saba.”
WALICHOSEMA MAJIRANI
WALICHOSEMA MAJIRANI
Baadhi ya majirani waliohojiwa na Uwazi
kwa masharti ya kutotaja majina yao walisema kwamba watu hao baadhi yao
walionekana wamezingira eneo hilo huku wakiwa na silaha nzito kwa ajili
ya kulinda usalama wa wenzao waliokuwa ndani kwa marehemu.
POLISI WANASEMAJE?
POLISI WANASEMAJE?
Baadhi ya askari polisi waliohojiwa na
Uwazi walisema maisha yao yako hatarini na kuiona kazi hiyo kwa sasa ni
chungu kwao kutokana na kuvamiwa, kuuawa na kunyang’anywa silaha kila
mara hali inayoifanya nchi itikisike.
“Kwa upande wetu polisi suala la ajira
si kama zamani kwani vijana wamekuwa wakichukuliwa hovyo kujiunga chuoni
bila kuzingatia sifa kama zamani. Kuna wahalifu wengi wameajiriwa na
wanatumiwa kufanya ukachero kwa manufaa ya vikundi vya uhalifu.”
MAREHEMU ALIKUWA DAR KWA AJILI YA KUTOA USHAHIDI
MAREHEMU ALIKUWA DAR KWA AJILI YA KUTOA USHAHIDI
“Marehemu alikuwa rafiki yangu na siku
moja kabla ya tukio aliniambia ametoka Morogoro kuja Dar kikazi ambapo
asubuhi ya Jumanne ya Agosti 4, (mwaka huu) alitakiwa kwenda kutoa
ushahidi Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwa kesi inayohusu kundi
fulani. Polisi kitengo cha uchunguzi wasimame imara watabaini kitu.
NI MFULULIZO
NI MFULULIZO
Mauaji ya kamanda huyo ni mfululizo wa
mauaji ya askari polisi nchini ambapo kwa kipindi kifupi tu, askari
waliouawa wanafikia saba.
KAMANDA WA POLISI
KAMANDA WA POLISI
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke, ACP
Andrew Satta ambaye alikuwepo katika kuuaga mwili wa marehemu ASP
Palangyo aliwaomba wananchi kutoa ushirikiano kwa vyombo vya usalama ili
kufanikisha kukamatwa kwa wahusika wote.
“Hili ni tukio la kinyama na hatuwezi kuvumilia hata kidogo. Tutahakikisha tunafanyakazi usiku na mchana na tutawakamata wote waliohusika na tukio hilo. Hakuna atakayepona. Naamini baadhi yao wako hapa wanatusikiliza,” alisema kamanda huyo.

Wakati gazeti hili linakwenda
mitamboni, Kamanda Satta alisema mpaka juzi watu watano wameshakamatwa
kufuatia mauaji hayo huku msako mkali ukiendelea. Kamanda Satta alisema
mwananchi mwenye taarifa zozote ampigie kupitia simu namba 0715 009979,
muda wowote.

Note: Only a member of this blog may post a comment.