Saturday, August 15, 2015

Anonymous

HALI TETE CCM!

Hali inazidi kuwa tete ndani ya Chama cha CCM baada  ya vigogo tisa, akiwamo Mwenyekiti wa Jumuiya ya UVCCM Vijana Mkoa wa Kilimanjaro (UVCCM), Fredy Mushi jana kujiuzulu nyadhifa zao na kutangaza kujiunga na CHADEMA. 

Wengine waliotimka ni Katibu wa Uchumi na Fedha na Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Taifa CCM, Paul Matemu, Mchumi wa UVCCM Mkoa wa Kilimanjaro, Jerome Komu na Noel Nnko ambaye alikuwa Mratibu wa Kanda ya Kaskazini wa Marafiki wa Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, wamo pia Wafanyabiashara maarufu wa mikoa ya Arusha na Kilimanjaro, Douglas Malamsha na Peter Kirenga. 

Kujitoa kwa vigogo hao, kumefanya idadi ya makada waliokihama CCM ndani ya mwezi mmoja kufikia 21. 
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye amesema CCM hakishtushwi na makada na viongozi wanaoendelea kukihama chama hicho na kujiunga na CHADEMA na kudai kuwa wanaoondoka wana sababu zao binafsi. 

Amesema hakuna kiongozi wa upinzani ambaye hakuanzia CCM hivyo ni hali ya kawaida kwa chama kikubwa kama hicho ambacho kina mtaji wa wanachama takribani milioni nane, makada wake kuhama.
“Waliohama, wanaohama na watakaohama hili siyo jambo jipya lilishatokea tangu miaka 23 iliyopita na litaendelea kwa muda mrefu hivyo siyo jambo la kushangaza, kuna viongozi wakubwa waliondoka na wengine wakarudi, Mfano Maalim Seif na Agustine Mrema walikuwa CCM na waliondoka”—Nape Nnauye. 

Nape alikanusha taarifa zinazosambaa mitandaoni kuwa, Mgombea urais wa CCM, Dk. John Magufuli, alitangaza kuwagawia kompyuta walimu wote.
Alisema taarifa hizo ni za uzushi na kwamba Ilani ya uchaguzi ya chama hicho ilipitishwa juzi mkoani Dodoma na inatarajiwa kuzinduliwa Agosti 23, mwaka huu.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.