Wednesday, August 19, 2015

Anonymous

HABARI NJEMA: Licha ya Kukana Kuwa Mjamzito Mdada SAJENTI wa BongoMovies Ajifungua!

sajenti
Msanii wa filamu Bongo, Husna Idd ‘Sajenti’.
Mwandishi Wetu
LICHA ya kukana mara kwa mara kuhusu kuwa na ujauzito, kuna madai kuwa msanii wa filamu Bongo, Husna Idd ‘Sajenti’ amejifungua mtoto wa kike.
Chanzo makini kililiambia gazeti hili kwamba mwanamama huyo alijifungua hivi karibuni katika Hospitali ya Kinondoni, maarufu kama Kwa Dokta Mvungi na kwamba jambo hilo analifanya siri kwani hataki watu wajue kama amepata mtoto huyo wa pili.
Gazeti hili lilipomtafuta na kumuuliza kuhusu madai hayo, alikataa katakata kuwa na mtoto, habari ambazo zimewashangaza watu wake wa karibu, waliosisitiza kuwa habari hizo ni za kweli na kwamba kwa sasa anaishi na mwanaye huyo kwa dada yake maeneo ya Sinza, jijini Dar es Salaam.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.