Gauni la staa wa filamu Bongo, Kajala
Masanja, lilizua minon’gono ukumbini wakati wa Shindano la Kinondoni
Talents Search (KTS) lililofanyika katika Ukumbi wa Millennium Tower,
Makumbusho jijini Dar baada ya gauni hilo kuambatana na watu wa
kulishika.

Staa huyo aliingia ukumbini hapo akiambata na kijana mmoja akilishika
gauni lake ambapo kila alipokatiza kijana huyo alikuwa na kazi ya
kuzunguka naye kuhakikisha nguo hiyo inakaa vizuri bila kujikunja kitu
ambacho kiliwafanya baadhi ya watu ukumbini kuanza kulishangaa gauni
hilo.
Kajala alipoulizwa sababu ya gauni hilo kushikiliwa alisema: “ Wale vijana ndiyo waliolibuni gauni langu ndiyo maana walikuwa makini kuhakikisha linakuwa sawa wakati wote,” alisema Kajala.

Note: Only a member of this blog may post a comment.