Bakteria wa Mycobacterium Tuberculosis (TB) anaweza kushambulia sehemu yoyote ya mwili, lakini mara nyingi hushambulia mapafu.
Watu wenye kifua kikuu kikali kwenye
mapafu yao wanaweza kuambukiza bakteria mtu mwingine yeyote anayekuwa
karibu yake kwani anapokohoa, kupiga chafya au kutema mate, mtu
aliyekaribu anaweza kuwavuta bakteria wa kifua kikuu wakati wa kupumua
na kuambukizwa.
Watu wanaweza kuambukizwa bakteria wa
kifua kikuu pia wasiokuwa wakali mwilini mwao. Iwapo mtu ana kifua kikuu
tulivu, ina maana kuwa mwili wake umefanikiwa kupambana na bakteria wa
maradhi hayo kikamilifu na kuwazuia wasisababishe ugonjwa.
Watu wenye kifua kikuu tulivu hawajisikii wagonjwa, hawana dalili, na hawawezi kuwaambukiza wengine.
Pata dondoo za afya za madaktari bingwa kwenye simu yako ya Vodacom bure: Tuma DAKTARI kwenda 15542
Note: Only a member of this blog may post a comment.