Ukijua sheria na haki yako ni rahisi kudai na kusimamia msimamo wako
kiuhalali kabisa. Hali ndivyo ilivyo kwa wamiliki wa nyumba nyingi huko
China ambao wengi ni wabishi hasa nyumba zao zinapotakiwa kubomolewa
kupisha miradi mbalimbali.
Je hapa kwetu watu wanajua sheria na taratibu zao? Picha hapo chini
zinaonyesha nchi ya kikomnisti ya China. Je nchi za kidemokrasia kama
tunavyojiita unaweza kufanya hivi?
Nyumba hii ya ghorofa iliyobomolewa nusu ikiwa ipo katikati ya mradi wa barabara huko Wenling, mashariki ya China katika jimbo la Zhejiang.
Mmiliki wa jengo hilo Luo Baogen, 67, akiwa na mkewe mwenye miaka 65
wamekuwa wakipambana kwa miaka minne ili waweze kupata dola za
kimarekani 41,300 kutoka serikali kufidia jengo hilo ili waweze kuondoka
hapo. Hali hiyo inaitwa nyumba misumari kwakuwa inakuwa ngumu kumtoa
kama hamjakubaliana naye na vile vile wana uwezo mkubwa wa kukuwajibisha
kisheria.
Nyumba msumari nyingine ikiwa katikati ya mtaa, kutokana na mwenye
nyumba hiyo kushindwa kuafikiana na serikali kuhusu malipo ili iweze
kubomolewa huko Nanning, Guangxi Zhuang.
Ghorofa hili ambalo ni la mwisho kwenye eneo la mradi likiwa na
bendera ya China huko jimbo la Henan. Inasemekana serikali ilishindwa
kufikia muafaka na mwenye nyumba hiyo na hivyo amegoma kuondoka mahali
hapo.
Gharofa hilo ambalo ni hoteli likiwa katika eneo ambalo linatakiwa
kujengwa soko kubwa la kibiashara katika wilaya ya Shenzhen. Mmiliki wa
jengo hilo Choi Chu Cheung, na mkewe Zhang Lian-hao, wametaka kulipwa
dola za kimarekani 2,327 kwa mita moja badala ya dola 840 kwa mita
ambazo zilipendekezwa hapo kabla na wamiliki wa mradi.
Na msumari huu mwingine ni katika eneo ambalo yanatakiwa kujengwa
makazi mapya ya kisasa ya kuishi lakini mmiliki wake ametaka kulipwa
fedha zaidi ndipo paweze kubomolewa, kulingana na vyombo vya habari vya
huko china.

Note: Only a member of this blog may post a comment.