Latiffah aka Tiffah hajamaliza hata siku moja lakini tayari ni staa
si tu kwenye mitandao ya kijamii na vyombo vya habari bali hata kwenye
midomo ya watu wanaofuatilia burudani barani Afrika.
Wazazi wake mwenyewe wanamuita ‘The Next Most Famous Daughter in
Africa.’ Kwa ukubwa wa Diamond Platnumz na mama yake Zari Ttale, hakuna
ubishi kuwa Tiffah ana kila sifa ya kuja kuwa ‘binti maarufu zaidi
barani Afrika.
Ikiwa ni saa chache tu tangu kuzaliwa kwake, akaunti yake ya Instagram iliyofunguliwa imefikisha followers zaidi ya 16,000.
Picha yake ya kwanza kuwekwa kwenye akaunti hiyo ina zaidi ya comments 860.
“Welcome to the next most famous daughter in Africa… my dad and mom
decided to call me Latiffah but I wanna be called Latty or Tiffah
#princesstiffa #lattyplatnumz,” yanasomeka maelezo kwenye picha hiyo.
Makadirio ni kuwa akaunti hiyo inaweza kuvuka followers laki moja
ndani ya siku mbili au zaidi ya followers 200k hadi wiki inaisha. Hiyo
ni speed kubwa sana kwa akaunti ya Instagram kupata followers kiasi
hicho.
Mashabiki wa Diamond na Zari na wana shauku kubwa ya kuiona sura ya
malaika huyo. Hakuna uwezekano wa wawili hao kuiweka sura yake mapema.
Hamu ya watu kutaka kumuona mtoto huyo inaweza kutumiwa kama fursa ya
kibiashara na wazazi wake.
Na pengine Diamond na Zari wanaweza kuwa miongoni mwa mastaa wachache
wa Afrika (kama wapo) waliowahi kuingiza fedha kupitia picha za mtoto
wao. Kipaji cha Diamond na Zari cha kutengeneza fursa za kibiashara
kinaweza kuwasaidia kumfanya mtoto wao kuanza kutengeneza fedha akiwa na
umri mdogo.
Kufunguliwa akaunti ya Instagram ni hatua ya kwanza katika kumbrand
mtoto huyo na kwakuwa mtandao huo umekuwa ukitumika kuwaingiza fedha
wasanii duniani, usishangae siku za usoni, makampuni makubwa hasa
yanayojihusisha na bidhaa za watoto, yakaichukua akaunti hiyo (retain)
ili waitumie kwenye promotion za bidhaa zao. Na isitoshe deals
zimeshaanza kuingia.
Tiffah
ndani ya masaa apata Endorsement na duka la watoto naenda kukamilisha
Terms na wahusika nitarudi na habari kamili… ππΎππΎ
— Daddie Dayyan (@Sallam_SK) August 6, 2015
Umaarufu wa mtoto wa kwanza wa Diamond si kitu ambacho
hakikutarajiwa. Habari kuhusu wapenzi hao kumkaribisha duniani mtoto wao
kwa siku kadhaa itatengenezwa vichwa vya habari katika bara zima la
Afrika. Kwenye mitandao ya kijamii hasa Instagram kwa siku mbili hizi Tiffah atakuwa haepukiki.

Note: Only a member of this blog may post a comment.