MABINGWA wa Kombe la FA, Arsenal leo wanajitupa uwanjani kukwaana na
mabingwa wa Ligi Kuu ya England, Chelsea kwenye mechi ya Ngao ya Jamii.
Mechi hiyo ya leo itapigwa kwenye Uwanja wa Wembley ikiwa ni maalum kwa ajli ya kufungua msimu mpya wa Ligi Kuu ya England.
Pambano la leo limekuwa gumzo kubwa miongoni mwa mashabiki wa soka
kutokana na mambo mengi ikiwemo suala la uhasama wa makocha wa timu hizo
Arsene Wenger na Jose Mourinho ambao wamekuwa wakiupiana vijembe kila
kukicha.
Wenger hajawahi kuifunga Chelsea ikiwa chini ya Mourinho kwa hiyo
mashabiki wanasubiri kwa hamu mpambano wa leo kuona kama historia hiyo
itavunjwa.

Note: Only a member of this blog may post a comment.