Monday, August 24, 2015

Anonymous

CHRIS BROWN anazidi kuonyesha mapenzi kwa mwanae, aamua kumpatia zawadi hii...

LAS VEGAS, NV - MAY 17: Singer Chris Brown and daughter Royalty arrive at the 2015 Billboard Music Awards at MGM Garden Arena on May 17, 2015 in Las Vegas, Nevada. (Photo by Gregg DeGuire/WireImage)
Msanii wa R&B Marekani Chris Brown siku hizi amekuwa mtu wa kuspend muda mwingi sana na mtoto wake wa kike, kila atakapo kwenda basi na mtoto Royalty yupo nyuma, sio siri mtu wangu ni wazi kuwa Chris Brown anaenjoy sana kuwa na kuitwa baba.
royalty3
Headlines za Chris Brown time hii kwenye kurasa za burudani ni ujio wa album yake mpya ambayo anategemea kuidondosha very soon, kizuri zaidi kuhusu album hii mpya ni jina aliloipa album hiyo!

Royalty Brown mtoto wa R&B Superstaa Chris Brown

Chris Brown kaamua safari hii awape mashabiki wake kitu tofauti, kitu kitakachowagusa mioyo ya mashabiki kama vile ambayo mtoto wake kaugusa moyo na maisha yake… kupitia Twitter page yake Chris alichukua time na kuandika maneno machache yaliosema; “Album yangu mpya itaitwa ‘ROYALTY'”.
royalty
Tarehe ya uzinduzi wa album hiyo bado haijafahamika ila kwenye interview moja aliofanya Chris Brown na mtangazaji maarufu wa Radio Ryan Seacrest, Chris alisema hii ni kama zawadi kwa mtoto Royalty ambaye kayabadilisha maisha yake, na aliye mfanya atake kuwa baba bora na mwanaume bora.
royalty2
Kwa sasa Chris ametoka kutengeneza video ya wimbo wake Liquor siku chache zilizopita na very soon itasogezwa kwetu mtu wangu, lakini kama hukubahatika kuusikia  basi nimekusogezea wimbo huo hapa chini.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.