Emeresiana Athanas
MGOMBEA urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk John Magufuli jana alichukua fomu za urais Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) huku viongozi wa chama hicho wakisisitiza kuwa ushindi kwa chama hicho ni lazima.
Dk. Magufuli alikabidhiwa fomu hizo saa 6.00 mchana Makao Makuu ya NEC yaliyopo katika makutano ya mitaa ya Ohio na Ghana jijini Dar es Salaam akiwa ameambatana na umati mkubwa wa watu wakiwa wamevalia sare za CCM.
Baada ya kukabidhiwa alirejea Ofisi ndogo za CCM Lumumba ambako viongozi mbalimbali wa chama hicho akiwamo Mwenyekiti wa Taifa, Rais Jakaya Kikwete walimpokea akiwa na mgombea mwenza, Samia Suluhu.
Akizungumza katika mapokezi hayo Mwenyekiti CCM Taifa, Kikwete alisema wanaodhani chama hicho ni cha mchezo watakiona cha mtema kuni kwenye Uchaguzi Mkuu ujao, kwani CCM kimejipanga vya kutosha kuhakikisha kinapata ushindi.
“Wanaodhani CCM ni chama cha mchezo watakiona cha mtemakuni na kama ni mpira basi watasimama kushuhudia magoli, tumejipanga na kama kushinda tutashinda.
Rais Kikwete alisema CCM kina uwezo na maarifa makubwa ya kushinda na kwamba kitamshughulikia hata aliye upande wa pili.
Rais Kikwete alisema chama hicho kinasubiri kufanya mkutano wa kutisha Agosti 22, mwaka huu na kwenye mkutano huo atashiriki mwenyewe hatamtuma mtu.
“Tumejipanga kwa hoja na tuna hakika tutashinda na tutaendelea kuzungumza zaidi mabaya na mazuri ya CCM ili Watanzania wayajue,” alisema na kuongeza kitaendelea kushinda kwani mambo yaliyofanyika chini ya Serikali ya chama hicho yapo na dunia inajua.
Akizungumzia shahada aliyopokea kutoka Australia, Rais Kikwete alisema imetokana na mambo makubwa yaliyofanyika ndani ya chama hicho katika kuleta maendeleo ya nchi.
Rais alisema kutokana na hatua hiyo imedhihirisha dhahiri kwamba hata nchi za nje zimetambua na kuona maendeleo hayo hadi kufikia kupewa shahada hiyo.
“CCM imefanya mambo makubwa, maendeleo yapo uhuru kwa vyombo vya habari upo, uhuru wa wanachama kuhamia chama kingine upo, hivyo kwa kuyaona hayo waliamua kunipa heshima ya pekee na kunipa shahada ya sheria ya juu kabisa,” alisema.
Mwenyekiti huyo wa CCM alisema kwa hali ilivyo sasa inaonesha watu wana tamaa kubwa na iliyokithiri kuvuka mipaka, pamoja na hali hiyo alisema chama kina uhakika wa ushindi na si wa hatihati.
Akizungumzia kuwepo kwake kwenye mapokezi hayo mara baada ya Dk. Magufuli kuchukua fomu, Rais Kikwete alisema kwenye shughuli, lazima na mwenye mtoto awepo, hivyo uwepo wake ni wajibu kwani yeye ndiye mwenye mtoto.
“Najua mtakuwa mkijiuliza uwepo wangu hapa, lakini uhondo wa shughuli na mwenye mtoto awepo, hivyo kwenye shughuli hii mimi ndiyo mwenye mtoto hivyo kuja kwangu ni wajibu kushuhudia kama kweli fomu zimechukuliwa,” alisema Rais Kikwete.
Kinana
Katibu Mkuu CCM, Abdulrahman Kinana, alisema katika uchaguzi wa mwaka huu chama kina uhakika wa kushinda, kwani wanashindana na makapi ya CCM.
“Nchi inaelekea kwenye uchaguzi, uchaguzi huo kutakuwa na mgombea na makapi ya CCM. Kwani aliyekuwa kule ni makapi, ametemwa huku amekimbilia huko na akimbilie huko huko.
Alisema kuwa kama upinzani ulianza na Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) na sasa utabadilika na kuwa Ukiwa.
Akizungumzia mapokezi ya Dk. Magufuli, Kinana alisema ni mazuri na kwamba ni dalili nzuri kwa chama hicho kupata ushindi wa kishindo.
Dk Magufuli
Akizungumza baada ya kuchukua fomu, Dk. Magufuli aliwashukuru wanachama kwa kumteua kuwania nafasi ya urais kupitia CCM.
Mgombea huyo alisema kutokana na mapokezi hayo ni dalili nzuri kwa chama kupata ushindi kwenye uchaguzi wa Oktoba 25, mwaka huu na kuendelea kutawala.
Dk. Magufuli alisema hana shaka na kugombea nafasi hiyo, kwani anazijua shida na mategemeo ya wananchi ukilinganisha na misingi iliyoachwa na Serikali ya Awamu ya Nne.
“Yapo mengi yamefanyika na nyie ni mashahidi, hivyo naomba niwahakikishie tu kwamba nitakuwa mtumishi wenu, kwani shida za wananchi nazijua,” alisema.
Alisema kwa sasa wananchi hawataki kero wala usumbufu na badala yake wanataka ajira, maendeleo, kukua kiuchumi, maisha mazuri na kubainisha kuwa atahakikisha anayasimamia na kuyatekeleza.
“Mimi nimekaa serikalini miaka 20 nikiwa mbunge na waziri na nimejifunza vya kutosha, hivyo nakuhakikishia mwenyekiti kwamba nimepokea kiti chako na nina uhakika tutashinda, kwani hakuna wa kutushinda,” alisema.
Aliongeza kuwa atapeperusha bendera ya CCM bila kubagua, kwani maendeleo hayachagui chama wala kabila, hivyo kwa umoja huo watashinda kwa kishindo.
“Misingi imara iliyojengwa na viongozi waliopita ni umoja wa Watanzania, hivyo kwa umoja huo nitakuwa mbele yenu kama mtumishi katika kuleta na kuangalia maendeleo ya Watanzania,” aliongeza Dk. Magufuli.
Mgombea huyo wa urais kupitia CCM alisema ataeleeza mengi kulingana na ilani ya chama hicho itakavyosema licha ya kuwa lengo kubwa ni kujenga uchumi wa Watanzania na kwamba viongozi waliopita hawakukosea.
Samia Suluhu
Kwa upande wake, mgombea mwenza wa Dk. Magufuli, Samia Suluhu Hassan alisema kutokana na mapokezi makubwa yaliyojitokeza kwenye msafara huo hakuna sababu ya CCM kushindwa na kuongeza chama kitahakikisha kinarudisha majimbo yote yaliyopo upinzani.
“Tunashukuru sana kwa mapokezi haya makubwa na katika uchaguzi huu tutajitahidi kurudisha majimbo yote CCM,” alisema.
Miongoni mwa wanachama waliokuwepo kwenye mapokezi hayo ni pamoja na Rais Kikwete, Kinana, Katibu wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Sadiki, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhani Madabida, mbunge Iddi Azan Zungu na Waziri wa Katiba na Sheria, Dk. Asha-Rose Migiro.
Wengine ni Waziri wa Habari Vijana na Utamaduni, Dk.Fenella Mukangara, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Hawa Ghasia, Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba na Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Stephen Wassira.
Mapokezi hayo yalisababisha shughuli za usafirishaji kwenye Barabara ya Mtaa wa Lumumba na Morogoro kusimama kwa muda kwa ajili ya kupisha msafara huo hadi kwenye ofisi za NEC jijini kutokana na umati wana-CCM waliowasili kumsindikiza Dk. Magufuli na Suluhu.
Katika ofisi za NEC ambako kulifurika wanachama wa CCM huku wengi wao wakigombania kuingia ndani jambo ambalo lilileta tafrani kati ya askari wa Jeshi la Polisi waliofika eneo hilo kuimarisha ulinzi.
Ulinzi
Hali ya ulinzi katika barabara hizo na ofisi za NEC uliimarishwa kwa kiwango kikubwa kutokana na idadi kubwa ya askari waliosambaa maeneo yote ambayo yalitumika kwa wakati msafari wa Dk. Magufuli ukipita.

Note: Only a member of this blog may post a comment.