Thursday, August 20, 2015

Anonymous

BREAKING NEWS: Jengo la Usalama wa Taifa Misri Lashambuliwa na Magaidi, 29 Wajeruhiwa

misri
Wananchi wakiwa eneo la tukio baada ya milipuko.
Takribani watu 22 wamejeruhiwa katika milipuko kadhaa ya mabomu iliyotokea katika ofisi za Usalama wa Taifa jijini Cairo, Misri mapema leo.
Vyombo vya habari vinavyomilikiwa na serikali ya Misri vimetangaza kuwa milipuko hiyo mitatu imetokea katika Wilaya ya Shubra al-Khaima.
watu
Wizara ya Afya ya Misri imetangaza kuwa watu 29 wamejeruhiwa katika milipuko hiyo ingawa vyombo vya habari vya kujitegemea vimesema ni mapema kuweza kujua idadi ya watu waliouawa au kujeruhiwa katika milipuko hiyo.
Watu sita kati ya 29 waliojeruhiwa ni polisi, Wizara ya Mambo ya Ndani Misri imeeleza.
Misri imekuwa ikilengwa kwa mashambulizi yanayofanywa na wanachama wa kundi la kigaidi la Daesh ambayo kwa kawaida yanalenga taasisi za serikali hususani ofisi na idara za polisi na usalama wa taifa.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.