Thursday, August 6, 2015

Anonymous

PICHAZ & VIDEO: LIONEL MESSI AMTWANGA KICHWA MCHEZAJI WA AS ROMA

Mshambuliaji wa kimataifa wa Argentina anaeichezea klabu ya FC Barcelona yaHispania Lionel Messi alishindwa kuzuia hasira zake baada ya kupigwa kikumbo naMapou Yanga-Mbiwa wa klabu ya AS Roma ya Italia, tukio hilo lilitokea katika mchezo wa kirafiki ambapo timu zote mbili zilikuwa zinautumia mchezo huo kama sehemu ya maandalizi ya mwanzo wa msimu.

Messi akiwa na hasira alimfuata Yanga-Mbiwa na kumpiga kichwa na mwamuzi aliwaonya kwa kuwaonyesha kadi za manjano wote wawili,mchezo ulimalizika kwa FC Barcelona kushinda kwa jumla ya goli 3-0 magoli ambayo yaliwekwa wavuni na wachezaji Neymer dakika ya 26, Messi dakika ya 41 na Rakitic akaitimisha goli la mwisho dakika ya 66 ya mchezo.


Nimekusogezea video ya tukio lenyewe

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.