Ofa iliyokubaliwa ya Manchester City kumsajili kiungo Raheem Sterling
kutoka klabu ya Liverpool imeweka rekodi mpya katika listi ya wachezaji
ghali zaidi wenye asili ya taifa la Uingereza.
Man city imekubali kuilipa Liverpool ada ya kiasi cha £49m kwa ajili
ya Sterling na kumfanya kuwa mchezaji ghali zaidi ambaye bado yupo chini
ya umri wa miaka 21.
Raheem Sterling sasa anashika nafasi ya pili nyuma ya Gareth Bale
aliyeuzwa miaka miwili iliyopita kwa ada iliyovunja rekodi ya Dunia ya
paundi millioni 85.3 – akitokea Tottenham kwenda Madrid.
Andy Carrol anashika nafasi ya 3 kwa kuuzwa kiasi cha paundi millioni 35 akitokea Newcastle kwenda Liverpool.
Rio Ferdinand alinunuliwa na Manchester United kutokea Leeds United
kwa £30m na kuweka rekodi ya kuwa beki ghali zaidi kwa kipindi hicho.
Listi kamili ya Wachezaji Ghali zaidi wa Kiingereza
85.3m – Gareth Bale (Tottenham to Real Madrid, 2013)
£49m* – Raheem Sterling (Liverpool to Manchester City, 2015) *subject to deal going through
£35m – Andy Carroll (Newcastle to Liverpool, 2011)
£30m – Rio Ferdinand (Leeds to Manchester United, 2002)
£27m – Wayne Rooney (Everton to Manchester United, 2004)
£26m – James Milner (Aston Villa to Manchester City, 2010)

Note: Only a member of this blog may post a comment.