Orodha ya wasanii watakaolishambulia jukwaa siku ya utolewaji wa
tuzo za MTV Africa Music Awards KwaZulu-Natal 2015 (MAMA) inazidi
kuongezeka.
Wasanii wa Afrika waliotajwa kuungana na kina Davido na Diamond, ni
pamoja na 2Face (Nigeria), Wizkid (Nigeria) (South Africa), Black Motion
(South Africa) pamoja Toofan (Togo).
Wasanii wengine wa Afrika ambao tayari wako kwenye orodha ya
kutumbuiza kwenye tuzo hizo ni pamoja na Yemi Alade (Nigeria), Cassper
Nyovest (South Africa) na Brucie (South Africa).
Kutoka Marekani atakuwepo Ne-Yo, rapper Young Thug, pamoja na muimbaji wa R&B JHENÉ AIKO.
Tuzo za MAMA zitatolewa July 18, 2015 Durban, Afrika Kusini.

Note: Only a member of this blog may post a comment.