Jana
July 15 2015 mmoja wa Wanasiasa wakongwe Tanzania mzee Kingunge
Ngombale Mwiru aliongea na waandishi wa habari na kusema hakuridhishwa
na kitendo cha CCM kutoliingiza jina la Edward Lowassa kwenye mchujo wa
kwanza wa Top 5 wa waliokua wanautaka Urais kupitia ticket ya CCM.
Mzee Kingunge alisema >>> ‘Kamati
Kuu inapelekewa orodha ya watu watano wapitishwe, hawa Wagombea wote 38
waliorudisha fomu hawakuwaona, hawakupita mbele yao, hawakuwauliza
maswali na hata kwenye Kamati ya Maadili naamini hawakuitwa..
Kuna watu
wachache wamekaa wakatengeneza orodha yao’
Pamoja na hayo, hii hapa chini ni video ikiwaonyesha Edward Lowassa,
January Makamba, William Ngeleja na Bernard Membe wakizungumza baada ya
Top 5 kutangazwa na list ikawataja January Makamba, Bernard Membe, Balozi Amina Salum, Asharose Migiro na John Magufuli.
-via millardayo

Note: Only a member of this blog may post a comment.