Leo ni siku nyingine tena, na inawezekana uchambuzi wa stori za magazeti leo Julai 16 kupitia @Clouds.Fm umekupita. Nimefanya jitihada ya kukusogezea stori zote za leo zikiwa na baadhi ya stori hizi kubwa…
Chama cha CUF imetaka viongozi wa chama hicho kusitisha zoezi la kutafuta mgombea Urais kupitia UKAWA mpaka suala hilo litakapo jadiliwa kikatiba ndani ya chama hicho siku ya Julai 25.
Viongozi wa dini waandaa maandamano kwa lengo la kumuomba Rais Kikwete kulifanyia mabadiliko Jeshi la Polisi, baadhi ya madereva wa boda boda wamkana jambazi wa tukio la Sitakishari wasema hakuwahi kuwa mwenzao.
Mtu anusurika kufa baada ya mguu wake wa kulia kuliwa na fisi akiwa usingizini, mtaro wa maji machafu imekuwa kikwazo Kawe na NEC imetaja mipaka ya majimbo mapya na mipaka mingine kukamilia baada ya sikukuu za Eid al-Fitr.
Matokeo ya kidato cha sita yametoka jana huku kijana Ramadhani Gembe aibuka kidedea wa Taifa kwa mwaka huu.
Sauti ya stori zote hizi iko hapa chini.

Note: Only a member of this blog may post a comment.