Waandishi Wetu,Dar es Salaam
HATIMAYE kigogo wa Simba, Zacharia Hans Poppe, ameamua kuzima utata uliokuwa ukienea katika ishu ya usajili wa mshambuliaji wao, Mganda, Emmanuel Okwi na kufafanua kuwa ameuzwa na si kwa majaribio kama taarifa zilizoenea hapo awali.
Awali, kulikuwa na mkanganyiko wa taarifa mbili tofauti, ambapo nyingine zilisema Okwi ameuzwa huku nyingine zikikanusha kwamba anakwenda kufanya majaribio katika Klabu ya Sonderjyske inayoshiriki Ligi Kuu ya Denmark.
Rais wa timu hiyo, Evans Aveva juzi akinukuliwa na chambo kimoja cha habari akisema kuwa mchezaji huyo kaenda kwenye majaribio ikiwa ni kauli sawa na aliyotoa mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Simba, Said Tully.
Lakini bosi wa kamati ya usajili wa klabu hiyo, amelithibitishia Championi Jumatano kuwa, mchezaji huyo kwa sasa si halali yao na kwamba wamemalizana kwa kila kitu na kufunguka zaidi kuwa, safari yake itakuwa ni kupimwa afya naakiwa fiti atasaini mkataba.
“Watu wanashindwa kutofautisha kati ya mchezaji anayekwenda kufanya majaribio na aliyeuzwa. Okwi haendi kufanya majaribio jamani, mtu aliyekwenda kwenye majaribio ni kama Mkude (Jonas), ila kwa Okwi tumefanya makubaliano na
timu hiyo na tukakubaliana kwa kila kitu.
“Yeye anakwenda kufanyiwa vipimo vya afya na akifuzu vipimo ndiyo itakuwa safari yake ya moja kwa moja na atajua
mwenyewe atasaini muda gani wa kuichezea timu hiyo,” alifunguka Hans Poppe.
Aidha, alisema Okwi alikuwa na mkataba wa mwaka mmoja na nusu ambao walimpatia baada ya ule wa awali wa miezi sita aliyosaini akitokea Yanga kufika kikomo.
Kauli ya kiongozi huyo mwenye mamlaka ya juu katika masuala ya usajili klabuni hapo, imefuta taarifa za baadhi ya viongozi klabuni hapo ambao wamenukuliwa wakisema kuwa amekwenda kwa majaribio ya siku 14.
Hans Poppe, alikwenda mbali na kutoboa siri ya ujio wa Hamis Kiiza ‘Aguero’ kwa kusema kuwa ni baada ya kusoma
alama za nyakati za Okwi kutimka.
wanza ishu yake siyo kwamba imekuja jana wala juzi, ila ni muda mrefu kama mwezi hivi umepita, walimtaka na tukakaa meza moja tukafikia muafaka kuhusu kumuachia. Kuona hivyo, tukaamua kumtafuta Kiiza haraka kama njia ya kuziba pengo lake,” alifunguka Hans Poppe huku akikataa katakata kutaja kitita alichouzwa.
Okwi anaingia kwenye rekodi za wachezaji waliozurura zaidi katika kipindi kifupi, ambapo tangu 2012 alitoka Simba kwenda Etoile du Sahel (Tunisia) kisha Villa ya Uganda, kabla ya kutua Yanga baadaye kurejea Simba na sasa Denmark.
Hata kama Simba imemsajili Kiiza lakini bado inaonekana kuwa itakuwa na pengo kubwa kutokana na uwezo mkubwa aliokuwa nao mshambuliaji huyo raia wa Uganda. WAANDISHI: Nicodemus Jonas, Martha Mboma na Khadija Mngwai

Note: Only a member of this blog may post a comment.