Friday, July 3, 2015

Anonymous

UNAFIKI TUPA KULE: VIDEO IPI KALI KATI YA HIZI?! DIAMOND PLATINUMZ vs ALIKIBA!

Diamond Vs Alikiba
Wasanii wawili, wote wanatokea mkoa ulibarikiwa kwa kuwa na vipaji, Kigoma, muimbaji wa ngoma ya “Cinderella” na muimbaji wa ngoma ya “Kamwambie” Alikiba na Diamond Platinumz, jamaa wanazidi kubreak the internet na kugonga vichwa vya habri mbalimbali hapa nchini na nje ya Tanzania. Wasanii hawa wanazidi kujitanua kimataifa kupitia muziki wao wanaoufanya.

Hivi karibuni kumuekuwa na sintofahamu kwa mashabiki kutokana na wasanii hao kukwea pipa hadi nchini South Africa kwenda kufanya vichupa vyao kila mmmoja kwa wakati wake.

Diamond alikwea pipa hadi kwa Afrika kusini na kufanya kichupa chake cha wimbo wa ‘’NANA’’ ngoma ambayo amemshirikisha msanii mkubwa kutoka Nigeria, Mr Flavour video ikiwa imefanywa na God Father na kichupa hicho kilipotoka kili-make headlines sana na kuleta gumzo kwa mashabiki na wadau wa muziki.

Alikiba nae alikuwa ametoa ngoma yake iliyofanya vizuri pia na kukamata charts mbalimbali, ngoma inafahamika kwa jina la ‘’CHEKECHA CHEKETUA’’ , Alikiba akaona sio kesi na yeye akakwea pia hadi kule kule kwa Madiba Afrika Kusini, alipofanya Diamond video yake ya ngoma ya “NANA”, “CHEKECHA CHEKETUA” iliongozwa na Meji Alabi na hatimaye kichupa kilitambulishwa katika kituo kikubwa cha Televisheni duniani cha Trace Urban siku ya Jumanne 30 Juni 2015.

Alikiba na Diamond ndio wasanii wa bongo flava wanaotazamwa sana kwa sasa kutokana ushindani uliokuwepo kati yao, ingawa kila mtu anakana kuwa hana tofauti na mwenzake,Mpaka imepelekea kutengeza makundi ya Team Diamond na Team Alikiba.

Sasa wewe ukiwa kama shabiki tuambie katika videos hizi mbili ‘’NANA’’ya Diamond na ‘’CHEKECHA CHEKETUA’’ ya Alikiba , Video Ipi Kali kuliko ya mwenzake , video zote zinapigwa katika vituo vikubwa vya TV duniani kama MTV BASE ,TRACE TV, Channel O na vingine.
Swali linakuja Video Ipi Kali kati ya “NANA” Ya Diamond feat Mr Flavor na “CHEKECHA CHEKETUA” ya Alikiba?

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.