Thursday, July 2, 2015

Anonymous

TATIZO la Kuharibika Kwa UJAUZITO-2


WIKI iliyopita tuliishia kwa kusema kuwa, kipindi cha ujauzito pia hugawanywa katika vipindi vitatu vilivyo sawa miezi mitatumitatu ambavyo kitaalamu huitwa ‘Trimesters’.

Kigezo kinachotumika kugawa vipindi hivi ni matukio yanayofanyika katika muda husika.
Kipindi cha uumbaji
Kipindi hiki huanza tangu mimba kutungwa mpaka miezi mitatu ya awali. Katika kipindi hiki ndipo viungo vya mtoto vinapoumbwa na kukamilika. Mimba inayoumbwa ikiwa na kasoro basi mwili wa mama unaofanya kazi vizuri huitoa wenyewe hapa tunaona ndio mimba inayotoka kabla ya miezi mitatu. Vyanzo vyake huwa ni nadra kutibika.

Vipo vyanzo vingi vinavyosababisha mimba changa ziwe zinatoka, vyanzo hivi ni rahisi kugundulika baada ya kufanyiwa uchunguzi wa kina na matibabu.

Cha kuzingatia hapa ni kwamba mimba nyingi zinazotoka katika kipindi hiki cha miezi mitatu ya kwanza mara nyingi chanzo huwa ni mimba yenyewe.Kuna wanawake wengi wana matatizo haya na hawajui kama tatizo hilo wanalo na wanaweza kutibiwa badala yake wanakazana kutafuta ujauzito badala ya kutafuta njia za kutatua tatizo hili la ujauzito kuharibika.

Kama una tatizo hili la ujauzito kuharibika au umetafuta ujauzito kwa muda mrefu bila kufanikiwa ni vema ukatembelea katika vituo vyetu ili ufanyiwe uchunguzi na kupata matibabu ya tatizo lako.

Tutaendelea wiki ijayo.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.