Wednesday, July 15, 2015

Anonymous

MZUKA WA SIASA WAZIDI KUWAPANDA WASANII TZ! HUYU NAYE ATANGAZA NIA!

Mzuka wa siasa unazidi kuwapanda wasanii wengi wa Bongo Flava. Hata hivyo Baba Levo hautaki ubunge bali ametangaza nia ya kugombea udiwani kupitia chama cha ACT – Tanzania katika kata ya Mwanga Kaskazini mkoani Kigoma.
baba-levo
Akizungumza na 255 ya XXL ndani ya Clouds FM, Baba Levo alisema anajipanga kuanzisha kitu kinachoitwa mgodi wa diwani.
“Ndani ya mgodi wa diwani kutakuwa na timu ya mpira, timu ya kuogelea, kutakuwa na timu ya mabondia, timu ya bongo movie na timu ya wanamuziki,” alisema. 

“Ndani ya mgodi kutakuwa na watu kama 200, baada ya kuwa na watu mia mbili, kwa sababu mimi ndo nitakuwa diwani na nitakuwa najua ni fungu gani limetoka kwaajili ya watu wa Mwanga Kaskazini, kwajili ya miradi mbalimbali yaani kazi zote zitakazohusu Mwanga Kaskazini, zitafanywa na timu ambayo ninayo mimi yaani Mgodi wa diwani. Yaani deal zote zinazokuja tutazifanya sisi,” aliongeza rapper huyo.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.