Thursday, July 2, 2015

Anonymous

MTANGAZAJI WA ITV, FARHIA MIDDLE AKIRI KULIZWA NA MAPENZI!


Mtangazaji wa ITV / Radio One, Farhia Middle.
Brighton Masalu MTANGAZAJI wa ITV / Radio One, Farhia Middle amesema tangu aujue ulimwengu wa mapenzi hajawahi kukutana na mwanaume mwaminifu na kwamba kila mara amekuwa akilizwa na mapenzi jambo ambalo husababisha kujiona mwenye mkosi. 

Akipiga stori na gazeti hili hivi karibuni, mtangazaji huyo alisema licha ya baadhi ya watu kumsifia kuwa ni mrembo kwa sura na umbo, lakini amekuwa akikutana na balaa la kuumizwa na mapenzi kwa kusalitiwa ama kunyanyaswa na wanaume.
“Yaani huwezi amini, wakati mwingine huwa najiuliza kwa nini mimi? Mbona kila mwanaume ninayempata sidumu naye. Kama siyo msaliti basi ni yule mwenye mfumo dume na hulka za kunyanyasa. Najiona kama nina mkosi,” alisema Farhia.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.