Monday, July 13, 2015

Anonymous

MSIBA: MKE AENDA KUJIRUSHA NIGHT CLUB, AFARIKI KWENYE AJALI MOROGORO! MUMEWE ALIKUA SAFARINI!

Rest in peace! Mwanamke, Glorian Zuberi ‘Fatuma’ amefariki dunia baada ya bodaboda aliyokuwa amepanda kugongwa na gari aina fuso, akitokea kujirusha.
Tukio hilo la kusikitisha lilijiri hivi karibuni, majira ya saa 8:00 usiku katika Barabara Kuu ya Morogoro-lringa eneo la Kwajeta jirani na Ukumbi wa Contena mjini hapa. 

Habari zilieleza kwamba mwanamke huyo alipokuwa kwenye ukumbi huo akila bata, alionekana kuwa kinara kwa kukata nyonga kila muziki wa sebene uliposikika huku waimbaji wa bendi iliyokuwa ikipiga ‘laivu’ wakilirusha jina lake kila aliponyanyuka kucheza. 

Ilidaiwa kwamba, mishale ya saa nane kasoro usiku, aliamua kutoka ukumbini hapo akiwa na mwanaume aliyedaiwa ni mchepuko na kukodi bodaboda kisha kupakizana ‘mshikaki’. 

Dakika tano baadaye, kiongozi wa bendi hiyo ya Maisha Mapya, Joshua Malekela alitangaza: ”Jamani hatuwezi kuendelea kupiga muziki, yule Fatuma aliyekuwa akicheza sebene amefariki dunia na watu wengine wawili baada ya bodoboda waliyokuwa wamepanda kugongwa na fuso.”
Baada ya taarifa hizo, mashabiki na mwandishi wetu aliyekuwa akisaka matukio, walifika eneo la tukio na kumshuhudi Fatuma, mwanaume aliyekuwa naye na dereva wa bodaboda wakiwa katikati ya barabara wamefariki dunia huku miili yao ikiwa imeharibika. 

”Kuna fuso lilikuwa likitokea Msamvu lilikuwa spidi kuelekea lringa ndipo dereva wa bodaboda aliyekuwa amepakia mshikaki alikata kona mbele ya fuso bila kuangalia nyuma wala kutoa ishara ndipo fuso likawagonga kwa nyuma na halikusimama,’’ alisema Juma Hamis, mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo.
Akizungumza na Ijumaa Wikienda, mama ma mzazi wa Fatuma, Etrapia Clemens alisema kuwa, siku ya tukio mwanaye alimuaga anakwenda ‘kupoteza mawazo’ kwenye Ukumbi wa Contena na wakati akireja nyumbani alipata ajali na kufa papohapo. 

Alisema miezi kadhaa iliyopita mwanaye alibadili dini na kufunga ndoa ya Kikristo na mumewe, William Mwalubuch ambaye wakati mkewe anakutana na umauti alikuwa safarini jijini Dar.
Marehemu Fatuma alizikwa katika Makaburi ya Wakristo ya Kolla mjini hapa.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.