July 14 2015 Dar es Salaaam
imemkaribisha Mgombea Urais ambaye amepitishwa na CCM pamoja na Mgombea
Mwenza… Hii ilikuwa safari ya kutambulishwa Mgombea Urais John Pombe Magufuli pamoja na Samia Suluhu Hassan ndani ya Dar baada ya Kikao Kikuu cha Halmashauri ya CCM kuwapitisha Wagombea hao Makao Makuu ya Chama, Dodoma Tanzania.
“Naomba
nirudie kushukuru Wajumbe wa Mkutano wa Taifa ambao waliamua kunipitisha
niwe Mgombea wa Urais nikiwakilisha CCM, ninawashukuru sana… Nilipokuwa
nachukua na kurudisha fomu mara nyingi nilikuwa nazungumza neno moja, ninaomba Watanzania waniombee…
Kupitishwa kwangu na Kamati Kuu inadhihirisha mlikuwa mnaniombea na
nataka niseme kwa dhati sitawaangusha, nitafanya kazi kwelikweli kama
nitapewa ridhaa kuiongoza hii nchi sitaogopa mtu na wala sitapenda mtu
wa chini aonewe kwa sababu maonevu yamekuwa yapo.”
“Nitahakikisha
ninaisimamia vizuri Serikali ili kero ndogondogo ziweze kufutika..
ndugu zangu sikuja kufanya Kampeni nilikuja kujitambulisha, jina langu
ninaitwa John Pombe Joseph Magufuli.” >>> Dk. Magufuli.
“Katika
Mchakato wa Chama tulikuwa Wanachama 42, na kulikuwa na Makundi 42 na
Makundi katika Kugombea sio makosa hasa kwa chama kama CCM, baada ya
Mchakato wote tumeungana na sasa tumekuwa group moja la CCM“
“Ninazungumza
jua linawaka haki ya MUNGU kweli tutafanya kazi, ninawaomba mkiamini
Chama cha Mapinduzi, niwaombe tushikamane kwa pamoja sura yangu ni
mbayambaya lakini saa nyingine inakuwaga nzuri usiku, sura ya tabia ni
nzuri lakini mnachohitaji ni kazi, maendeleo na kuondolewa kero zao..
mimi sio mkali ila nawachukia watendaji ambao hawatimizi wajibu wao, na
hao ndio nitalala nao mbele.“>>> John Magufuli.
Utamsikiliza hapa Waziri Magufuli wakati akiongea na watu wa Dar baada ya Mapokezi yake July 14 2015.

Note: Only a member of this blog may post a comment.