Friday, July 31, 2015

Anonymous

MAKAVU LIVE: Kifo cha Bobby Christina, mastaa mateja TZ mna hamu nanyi yawakute?!

bobbi-kristina-b-768Marehemu Bobbi Christina.
JUMAPILI iliyopita, mtoto pekee wa waimbaji nyota wa muziki nchini Marekani, Whitney Houston na Bobby Brown aitwaye Bobbi Christina, alifariki dunia baada ya kuwa amelazwa tangu Januari mwaka huu, akiwa hajitambui. 

Bobbi, ambaye wazazi wake wote wawili walikuwa ni waathirika wa madawa ya kulevya, Januari 31, mwaka huu alikutwa ameanguka bafuni nyumbani kwake akiwa hajielewi na uchunguzi wa kitabibu ulionesha kwamba alianguka baada ya matumizi makubwa ya madawa ya kulevya, ambayo pia yalisababisha kifo cha mama yake mzazi, Whitney, Februari mwaka 2012.
RayCCCCC.jpg 
Ray C
Tangu wakati huo hakuweza kujitambua na katika wiki za hivi karibuni wakati akipigania maisha yake kwa kusaidiwa na mashine, ndugu zake walikizunguka kitanda chake, wakisubiri miujiza ya Mwenyezi Mungu kuweza kurejesha uhai wa msichana huyo mdogo, aliyezaliwa Machi, 1993.
Mamlaka nchini Marekani zinamtaja mpenzi wake, Nick Gordon ambaye awali alimfahamu kama kaka yake kutokana na kuishi katika familia yao kwa muda mrefu, kuwa ndiye alikuwa kinara wa kumfundisha utumiaji wa madawa hayo na hivi sasa amewekwa sehemu ya uangalizi kwa ajili ya usalama wake!
CHIDBENZ.JPGChid Benz
Nimeanza hivi ili kuendelea kuwaasa vijana wetu wasanii ambao kwa ulimbukeni au kuiga, wamejikuta wakiwa wateja wakubwa wa kutumia madawa ya kulevya. Tunawajua hawa ninaowazungumzia, baadhi yao tumewapoteza, wengine wako mahututi na waliobaki, hawako salama.

Kinachowasumbua ni ushamba tu, wa kutaka kufanana staili ya maisha na vijana wenzao wa Marekani. Wanatumia madawa ya kulevya huku wakijua wazi madhara yake.

Wanawaona wapiga debe wengi jinsi wanavyopoteza mwelekeo wa maisha yao kutokana na tabia hii, lakini unashangaa kumuona kijana ambaye tayari ameshajiajiri kwa muziki, anatumia sehemu ya pato lake kupoteza dira yake.

Mtu mjanja hawezi kutumia pesa yake kujiangamiza. Uvutaji unga ni ujinga kwa sababu mwisho wa siku huwafanya watumiaji kuwa wajinga. Kwa sababu akili zao zinaharibika.

Utawakuta wakiwa wadokozi wa vitu vidogo kama vijiko vya ndani, deki za video, chenji zinaachwa mezani, mashuka, mapazia au hata kupora wanawake.

Na kitu kingine wasichokifahamu ni kwamba wakati watumia unga wasanii wa Marekani wanaishi angalau vizuri kutokana na mfumo wa malipo ya kazi zao kuwa mzuri, huu wa kwetu ni mbaya ambao kama mtu hapati kazi za mara kwa mara, ni vigumu kupata fedha za kuweza kujimudu kimaisha, achilia mbali pesa ya kununua hicho kitu.

Ndiyo maana utawaona wasanii wetu watumiaji wa unga wanabadilika kiasi cha kututia shaka, afya zao hunyong’onyea na huwa wakali wakiulizwa kulikoni.

Rehema Chalamila ‘Ray C’ anafahamika kuwa anatumia dawa za kuondoa athari za unga mwilini na tunakumbuka jinsi Chid Benz alivyokamatwa na ‘kete’ pale uwanja wa ndege.

Tunao vijana wengi tu ambao wanatambulika kuwa wanatumia unga. Ni vyema nikawarudia tena kuwaeleza kuwa mwanzo wa matumizi ya unga ni mwisho wa matarajio ya mafanikio yao kimaisha. Ingawa kila mmoja anaishi kwa namna anavyoamini, siyo jambo zuri kumuacha mwenzio akipotoka katika ustawi wa maisha yake.

Hata kama tuna wivu kama dhambi ya asili ya binadamu, lakini haipendezi unapomuona kijana aliyestahili kuishi vizuri, akivaa vyema, akiwa katika usafiri wake mzuri na mwenye makazi ya thamani, akiishi kama ombaomba mtaani kwa sababu tu, tuliamua kukaa kimya tulipomuona anaanza kupotea.

Kama wewe unamjua jirani, ndugu au jamaa anayetumia unga, mpe mfano wa binti huyu ambaye alikaa miezi sita hospitalini akiwa hajitambui hadi mauti yalipomkuta!

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.