Friday, July 31, 2015

Anonymous

MAJONZI TELE: MASTAA WAMLILIA BOBBI KRISTINA!

Marehemu Bobbi Kristina enzi za uhai wake.
New York, Marekani
INASIKITISHA SANA! Baada ya kifo cha mtoto wa staa wa R&B, Hayati Whitney Houston, Bobbi Kristina aliyefariki dunia mwishoni mwa wiki iliyopita, mastaa wengi nchini Marekani wameonesha hisia zao za kuguswa na kifo hicho kwa kutuma salamu za pole kuifariji familia ya marehemu.

Keri Hilson.
Baadhi ya mastaa waliotuma salamu za rambirambi kwa familia ya Bobbi Kristina ni pamoja na Keri Hilson, Missy Elliott, Nick Minaj na wengine wengi.
Bobbi ambaye mama yake, Whitney Houston aliyefariki Februari, 2012 alianza kuzidiwa tangu Januari 32, mwaka huu alipokutwa amedondoka bafuni huko nyumbani kwao Atlanta, Marekani huku ikidaiwa alizidisha matumizi ya madawa ya kulevya.
Kutokana na hali yake kuendelea kuwa mbaya mwezi uliopita familia yake ilimuondoa kwenye tiba na kumrudisha nyumbani hadi pale umauti ulipomkumba akiwa na umri wa miaka 22.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.