Monday, July 13, 2015

Anonymous

Majibu ya DULLY SYKES Kuhusu Kuchukua Uamuzi Kama wa ALI KIBA!


Msanii wa muziki, Dully Sykes amechukua uamuzi mgumu kama uliofanywa na msanii mwenzake Ali Kiba kwa kuto kumfollow mtu yoyote kwenye akaunti yake ya instagram.

Dully ambaye akaunti yake imefikisha followers 158K amezungumza na millardayo.com na kusema...’Mara nyingine utakuwa labda nina wafollow mastaa wenzangu au mtu yoyote hao hao utakuta kuna wakati wanapost vitu vinavyonikera mimi hiyo ndio sababu kwa hiyo nitaanza ku follow media mbalimbali kama CNN, MTV na media zingine zote nitazi follow ili niwe napata habari tofauti lakini sio kumfollow msanii mwenzangu au kumfollow mtu ambaye najua anayejihusisha na hivyo vitu mwisho wa siku aje kunipandisha pressure‘ – Dully Sykes

‘Mimi pia nitukanwa ni kati ya watu ambao wanaotukanwa japo situkanwa sana kama hivyo unavyofikiri lakini sasa ninavyotukanwa ninakuwa naambiwa kuwa kuna watu hivi na hivi wamenitukana kwa hiyo bora nisikie kuliko kuona kwa macho’ – Dully Sykes.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.