Wakati Bastian Schweinsteiger, Matteo Darmian na Morgan Schneiderlin
wakielekea Old Trafford kukamilisha ndoto zao za kujiunga na moja ya
vilabu vikibwa duniani, Robin van Persie yeye ameondoka kwenye klabu
hiyo.
Mshambuliaji huyo jana alisafiri kwenda Istanbul na alipokelewa kama mfalme na mashabiki wa klabu yake mpya.
Van
Persie ambaye aliiwezesha United kushinda ubingwa wa 20, akifunga
magoli zaidi ya 20, msimu uliopita alikumbwa na balaa la majeruhi
akiishia kufunga magoli 10 tu.
Fenerbahce walithibitisha Alhamisi kwamba wameingia kwenye mazungumzo na United juu ya uhamisho wa ndachi huyo.
Van Persie sasa anaungana na mchezaji mwenzie wa zamani wa United, Luis Nani.

Note: Only a member of this blog may post a comment.