Monday, July 13, 2015

Anonymous

MAGUFULI Atangaza VITA na Watu Hawa!

Akihutubia mamia ya wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma jana baada ya kupitishwa na CCM kuwania urais, Dk. Magufuli alitangaza vita ya kupambana na wazembe, mafisadi, wala rushwa na wabadhirifu kuwa atapambana nao kwa nguvu zake zote.

Dk. Magufuli alisema: “Wazembe na wabadhirifu watakaokuwa pamoja na wezi na wala rushwa nitawashughulikia kwa upole sana. Nitalinda uhuru wa mipaka yetu kwa kuwa ni ya watu wote ingawa nita-deal na mtu atakayehatarisha uhuru wetu…Watanzania najua wana matumaini makubwa na mimi.” 

Aidha, mgombea huyo aliwaeleza wakazi wa Dodoma kuwa iwapo atapewa ridhaa na Watanzania kuwa Rais wa Tanzania atahahikisha vijana wanatatuliwa changamoto za ajira kwa haraka na kwa kasi zaidi.

“Nataka niwahakikishie Watanzania na wana -CCM kwa ujumla kwamba CCM ipo tayari kwa mageuzi ya uhakika na ya haraka kwa watu wote. Sitawaangusha Watanzania na vyama vingine vyenye itikadi tofauti na Chama cha Mapinduzi,” alisema na kushangiliwa na wananchi waliohudhuria mkutano huo.

Aliwapa matumaini wanachama waa chama hicho kwamba hatawaangusha kwani dhamana aliyopewa ni kubwa hivyo atahakikisha CCM inapata ushindi mkubwa wakati wa uchaguzi mkuu.

“Leo ni siku muhimu katika chama chetu, hata kwangu mimi mwenyewe… naona ni siku muhimu. Sitawaangusha Oktoba..narudia tena sitawaangusha…hata wale wa vyama vingine sitawaangusha, ” alisema na kuongeza.” 

“Nitatekeleza mambo yote yaliyomo ndani ya ilani ya uchaguzi kuhusu masuala ya barabara, viwanja vya ndege, maji, umeme na mengine nitahitaji sana msaada kutoka kwenu.”

Dk. Magufuli katika mkutano huo alitambulishwa na Rais Jakaya Kikwete, muda mfupi baada ya kutangazwa matokeo yaliyompa ushindi wa kupeperusha benderea ya CCM wakati wa uchaguzi mkuu dhidi ya vyama vya upinzani.

Baada ya kuchaguliwa na Mkutano Mkuu wa CCM kuwa mgombea urais wa chama hicho, Dk. Magufuli alimteua Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, anayeshughulikia mambo ya Muungano, Samia Hassan Suluhu kuwa mgombea wake mwenza.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.