Monday, July 13, 2015

Anonymous

LOWASSA Atibua Mazoezi SIMBA SC



Aliyekuwa mgombea mtarajiwa wa urais nchini kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Edward Lowassa.
Na Omary Mdose, Lushoto
BAADA ya aliyekuwa mgombea mtarajiwa wa urais nchini kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Edward Lowassa jina lake kukatwa kwenye nafasi hiyo, hali ilibadilika kwenye mazoezi ya Simba yaliyofanyika juzi Jumamosi kwenye Uwanja wa Chuo cha Magamba, Lushoto, Tanga.


Wachezaji wa timu ya Simaba wakiwa mazoezini.
Jina la Lowassa lilikatwa usiku wa kuamkia Jumamosi ambapo awali wachezaji na makocha wa Simba walipofika uwanjani hapo kwa ajili ya mazoezi walikuwa hawajapata taarifa zozote kuhusiana na jambo hilo ambapo shabiki mmoja aliibuka na kusema kwa nguvu ishu hiyo ndipo kila mmoja wao akashtuka.

Championi Jumatatu ambalo limeweka kambi maeneo haya, lilishuhudia tukio hilo ambapo baada ya kila mmoja kupata taarifa hizo akaanza kusema lake. 

Wapo waliokuwa wakishangilia huku wengine wakikasirika ambapo wakati mazoezi yakiendelea jina la Lowassa lilikuwa likitajwa kila wakati hali ambayo iliwashtua wengi.

Hawakuishia hapo kwani waliendelea kutaniana huku wengine wakiitwa timu Lowassa ambapo kitendo hicho hakikukasirikiwa na kocha bali ilichukuliwa kama utani tu.
CCM imempitisha Dk John Pombe Magufuli kuwa mgombea urais kwa tiketi ya chama hicho.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.