Saturday, July 11, 2015

Anonymous

KIMENUKA! LOWASSA ALETA MPASUKO CCM, NI BAADA YA KUKATWA JINA KWENYE TANO BORA!

Habari za kutoka makao makuu ya CCM mkoani Dodoma ni kwamba wajumbe wa kamati kuu watatu ambao ni Dkt. Emmanuel Nchimbi, Sophia Simba na Adam Kimbisa wamepinga maamuzi ya kamati ya kumkata mmoja wa wagombea maarufu na kumweka mgombea asiyekuwa maarufu.

Akizungumza usiku huu majira ya saa saba za usiku Dkt. Nchimbi amesema kwamba wao watatu hawajakubaliana na maamuzi ya kamati kuu iliyoketi usiku huu chini ya Mwenyekiti Dkt Jakaya Kikwete kumkata mgombea maarufu kwa manufaa ya mgombea asiye maarufu.

“Katika kikao cha leo kamati haikupoea majina yote yaliyojadiliwa na maadili, suala ambalo ni kinyume na kanuni, pili katiba ya CCM inataka mtu anayekubalika ndiye apewe nafasi ya kwanza, lakini kikao cha leo kimeonyesha kuminya wanaokubalika kwa manufaa ya wachache wasiokubalika” Amesema Dkt. Nchimbi.

Hivyo basi kwa sababu hiyo wao watatu ambao ni wajumbe wa kamati kuu wamewataarifu wenzao kwamba wamejitenga na maamuzi ya kikao hicho na kutangaza kuto kuyaunga mkono.

Kwa mujibu wa tafiti mbalimbali za kisiasa nchini Tanzania zinaonesha kuwa mgombea anayekubalisa sana CCM ni Mbunge wa Monduli Edward Lowassa akifuatiwa na Waziri wa Mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa Bernad Membe.
Tazama video Nchimbi akifunguka live hapa 

CCM VIPANDE VIPANDE MAJINA MACHACHE YAPELEKWA KAMATI KUU MENGINE YAONDOLEWA KINYEMELA BAADHI YA WAJUMBE WA KAMATI KUU HAWAKUBALIANI NA MAAMUZINape katoka na kutangaza majina bado yanafanyiwa kazi. Yatarudishwa kesho saa 4 White House kwenye kikao cha Halmashauri Kuu. John NchimbiSophia SimbaAdam KimbisaWametoka na kutoa tamko kwamba hawakubaliani na maamuzi ya wajumbe wenzao. Wanasema majina waliyoletewa ni baadhi tu. Hawajataka kuzungumza zaidi
Posted by Zanzibar Post on Friday, July 10, 2015

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.