Monday, July 27, 2015

Anonymous

Kama ulikuwa unasubiri Big Brother Africa 2015 kwenye TV yako, ikufikie hii taarifa kuhusu Shindano hilo

Kumekuwa na uvumi mkubwa juu ya shindano kubwa la TV Africa, Big Brother Africa (BBA) kutokufanyika mwaka huu na inadaiwa sababu ni ukosefu wa wadhamini wa shindano hilo.

Waandaaji wa shindano hilo, Africa Magic na Endemol wamesema shindano hilo la BBA 2015 linaweza lisifanyike mwaka huu na hivyo kuahirishwa mpaka mwakani.

Richard Bezuidenhout mshindi wa kwanza kutoka Tanzania wa Big Brother Africa II 2007
Manager wa Multichoice Ghana, Anne Sackey amethibitisha uvumi wa taarifa hizo kwa kusema kuwa wao Multichoice Ghana walipokea taarifa kutoka MNET kuwa shindano la BBA mwaka huu halitofanyika kama ilivyozoeleka.

Mshindi wa pili kutoka Tanzania wa Big Brother Africa Hotshot 2014; Idris Sultan.
Anne Sackey amesema kuwa MNET hawajatoa sababu za kwanini shidano hilo halitofanyika mwaka huu lakini kwa upande wake anaamini kuahirishwa kwa shindano hilo ni kutokana na ugumu wa kupata wadhamini kwani kuendesha kipindi hicho hugharimu pesa nyingi sana.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.