STAA wa filamu Bongo, Adam Haji ‘Baba Haji’ juzikati
aliangusha sebene la nguvu kwenye Viwanja vya Ngome Kongwe, Zanzibar
baada ya kupata taarifa kuwa staa wa kike nchini aliyekuwa akiwania
nafasi ya ubunge wa viti maalum mkoani Singida kwa ‘leseni’ ya Chama Cha
Mapinduzi (CCM), Wema Isaac Sepetu ameangushwa.
Wema Sepetu.
Akionekana mwenye furaha huku
akiserebuka muziki alisema kuwa mbunge wenu amekosa ubunge, jambo
lililowafanya baadhi ya wasanii wenzake waangue kicheko kwa kuwa
inafahamika kuwa ana bifu naye.
“Jamani mmesikia majibu? Mbunge wenu
kashika nafasi ya mwisho, ngoja mimi niendelee kucheza sebene langu,”
alisikika Baba Haji huku akiangua kicheko.
Bifu la Baba Haji na Wema lilianza
kitambo ambapo wawili hao walikutana kwenye Ukumbi wa Bilicanas, Posta
jijini Dar ambapo Wema alimchana jamaa huyo kuwa ananuka jasho.

Note: Only a member of this blog may post a comment.