Team ya Hekaheka leo ilikua eneo la
Ununio nje kidogo ya jiji la Dar es salaam baada ya kupigiwa simu na
watu kuhusu jirani yao ambaye alikuwa anakula kupita kiasi, kitu ambacho
si cha kawaida.
Mwenyewe amesema anaona ni kipaji
alichojaliwa na Mungu kwa kuwa na uwezo wa kula zaidi ya mtu wa
kawaida..anasema kwa siku anamaliza kilo nne akimaanisha asubuhi
anatumia kilo moja ya mchele, mchana unga kilo moja na jioni hivyo
hivyo.
Anasema asubuhi akishindwa kula wali
basi hula chapati 25 au maandazi 50, pia ana uwezo wa kumaliza soda 15
kwa wakati mmoja..na humfanya kuweza kufanya kazi yoyote ambayo atapata
kwa siku hiyo.
Msikilize mwenyewe hapa akihojowa na Geah Habib…

Note: Only a member of this blog may post a comment.