Kada wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Kingunge Ngombale,Mwilu (kushoto) akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo ,Kuhusu mkutano mkuu wa chama hicho uliofayika Dodoma hivi karibuni na mchakato wa kumpata mgombea Urais na changamoto zilizojitokeza.

Mwanasiasa Mkongwe nchini,Kingunge Ngombale Mwilu akisisitiza jambo mbele ya Waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali (hawapo pichani) mapema leo,nyumbani kwake makumbusho,jijini Dar.
PICHA NA MICHUZI JR. .
Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii .
Mwanasiasa mkongwe nchini,Kingunge Ngombale Mwilu amesema kuwa wanachma wa Chama cha Mapinduzi (CCM) ,umefika wakati muafaka sasa wa kuungana pamoja na kuzika tofauti zao zilikuwa zikijitokeza hapo awali badala yake wasimame imara kukijenga chama chao.
Akizungumza na waandishi habari leo jijini Dar es Salaam,Kingunge amesema CCM inatambulika kimataifa kutokana na historia yake,hivyo lazima kiwe imara wakiwemo viongozi wake wakiwashirikisha na wanachama wao .
Amesema katika uchaguzi wa kutafuta mgombea urais uliofanyika hivi karibuni mkoani Dodoma ulikiuka haki za wagombea kutokana na wagombea kushindwa kwenda katika Mkutano mkuu wa wanachama na kujieleza.
Kingunge amesema ,kilichotokea Dodoma sio halali na sio haki lakini chama cha CCM lazima kiendelee,alisem na kuongeza kuwa "tumepata mgombea John Magufuli yeye sio aliyefinyanga na wajumbe wa mkutano mkuu,hivyo tumuunge mkono kwa pamoja na kupata ushindi wa kishindo",alisema Kingunge.
"Wana CCM watafute umoja wa kushikamana na kuwa Lowassa ana nafasi ndani ya CCM,hivyo tuunde mazingira ya kutumia nguvu zilizopo CCM katika kushinda kwa ushindi wa kishindo katika uchaguzi mkuu",amesema Kingunge.
Amesema yaliyotokea Dodoma lazima yazungumzwe ili watu waweze kutoa duku duku zao kwa kile ambacho kimeonekana katika chama na ni changamoto kubwa ambayo inapaswa kufanyiwa kazi.

Mwanasiasa Mkongwe nchini na Kada wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Kingunge Ngombale Mwilu (kushoto) akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo ,Kuhusu mkutano mkuu wa chama hicho uliofayika mjini Dodoma hivi karibuni na mchakato wa kumpata mgombea Urais na changamoto zilizojitokeza

Note: Only a member of this blog may post a comment.