SOKO la Wakulima lililoko Mtaa wa Majengo, wilayani Kahama mkoani
Shinyanga limeteketea kwa moto usiku wa kuamkia leo majira ya saa nane.
Chanzo cha moto huo kinadhaniwa kuwa ni shoti ya umeme iliyotokea kwenye
jengo hilo, hivyo kusababisha jengo lote kushika moto na kuungua hadi
kuteketea.
Kwa mujibu wa shuhuda wa tukio hilo ni kwamba hakuna mtu aliyefariki wala kujeruhiwa kutokana na moto huo..

Note: Only a member of this blog may post a comment.