Tuesday, June 16, 2015

Anonymous

YOUNG DEE: Niliwahi kujutia umaarufu wangu!

Rapper Young Dee amesema amewahi kujutia kuwa mtu maarufu kutokana na kukosa pesa zinazolingana na jina lake.
11280269_1585554741708067_937645765_n
Akiongea na E-News ya EATV, Young Dee alisema,” Tokea nimekuwa Young Dar es Salaam, sijawahi kujuta lakini nilijuta nilivyokuwa Young Dee mwanzo wakati naanza. Si unajua ndo nilikuwa nimetoa ngoma yangu ya kwanza halafu bado sina kitu alafu inabidi upande daladala halafu unakutana na madenti wamekaa siti ya nyuma wanaanza ‘Young Dee’ wanazingua kweli yaani.” 
 
“Ile ilikuwa inanitesa sana maana nilikuwa naona nashindwa kuwa huru na maisha yangu yaani kuwa mtu wa kawaida tu nikapanda daladala nikakaa poa tu. Lakini ilikuwa ngumu hiyo hali ilikuwa inanitesa sana kipindi cha nyuma.”
-bongo5

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.